Sunday, August 12, 2012

HABARI ZOTE NA N LUCAS RAPHAELTABORA



Mkuu wa wilaya ya sikonge mkoni Tabora  Hanifa Selengu amewataka watumishi wa wilaya hiyo kufanya kazi kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuepuka matatizo yanayoweza kuwapata kwa kukwepa kutozifuata sheria hizo .

wito huo aliutoa wakati akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo kwa mara ya kwanza mara baada ya kuteuliwa na Rais kushika wadhifa huo katika wilaya hiyo.

Aliwataka watumishi wote wafanye kazi kwa ushirikiano ,ikiwa ni pamoja na kushirikiana na madiwani katika shughuli zote za maendeleo katika kata zao kwa ajili ya kufuatilia na kutathimini.

Hanifa amewataka watendaji wa vijiji na kata kuwahimiza wananchi katika sehemu zao kujumuika kwenye usafi wa mazingira ili kuepuka magonjwa yanayoweza kuwapata wananchi bila ya wao kutambua.

Alisema kuwa kila jumamosi iwe siku ya usafi katika wilaya ya sikonge ikiwa ni usafi wa vyoo ,mazingira yanayozunguka maeneo ya biashara ,nyumba na mifereji ,ambapo sheria ndogo zitatumika kwa ajili ya kuchukulia hatua watu wakaokaidi .

Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka wakuu wa idara nawatendaji wa kata katika halmashauri ya wilaya ya sikonge  na watumishi wa chini yao kufanyakazi  kama timuya ushindi kwa kufuata sheria kama zilivyowekwa na serikali za mitaa .

Hanifa alendelea kusistiza watumishi kufanya kazi kwa bidii,kujituma na kutoa mrejesho wa shughuli zao na kuwataka kuwahamasihsa wananchi wa wilaya hiyo ambapo kila kaya kuwa na mpango kazi wa maendeleo .


Ametoa onyo  kwa watendaji wanajifanya kuwa mungu watu bali watumishi wote wa wilaya hiyo ni watumishi wa wananchi na kuwaletea maendeleo.

Mwisho

WANAWAKE.

Vikundi vya wananwake katika halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora wametakiwa kufanya kazi kwa nguvu zote ili kuweza kutimiza azima ya vikundi hivyo kuwaletea maendeleo wao ,familia zao na taifa kwa ujumla.

Ushauri huo ulitolewa na mkurungezi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge ,Paul Nkulila katika halfa fupi ya kutoa mikopo kwa vikundi vya kimama  katika ukumbi wa halshauri huyo ambapo vikundi 12 vyenye wananwake 120 walipatiwa kiasi cha shilingi milioni 12.

Alisema kwamba vikundi hivyo vya kinamama vinapaswa kurejesha  mikopo hiyo kwa kipindi walichofunga mkataba ili kuwezesha wananchi wengine waweze kupatiwa mikopo hiyo kwa ajili ya kusukuma maendeleo kwa wanawake .

Mkurungezi huyi wa halmashauri ya wilaya ya sikonge amewataka maafisa maendeleo ya jamii kuvitembelea vikundi hivyo mara kwa mara na  kuvishauri jinsi ya uzalishaji katika biashara zao .

Aidha Nkulila amewataka wananwake hao kuwa na upendo miongoni mwao na wazidishe mshikamano na siyo kila mtu anafanya kazi kivyake vyake upendo ni lazima ,kwanimkufanikiwa kwa mwanamke mmoja wao ni mafanikoa makubwa kwa wanawake wote wa wilaya ya sikonge.

Awali akitoa taarifa kwa mkurungezi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya sikonge ,afisa maendeleo ya jamii, Hemistocles Byarugaba alisema kwamba idara hiyo ya maendeleo ya jamii imevitembelea  vikundi mbalimbali ilivyoomba mikopo ili kudhibitisha kuwa wanayo miradi waliyoombea mikopo na dida hiyo imefuatilia mara kwa mara urejeshai wa mikopo kwa waliokopa katika vipindi tofauti.

Alisema kwamba ameitaja baadhi ya miradi iliyoombea mikopo kuwa ni migahawa ,kilimo,biashara ,vioski na maduka .

Mingine ni vikundi vya ushonaji na wa vyerehani,na biashara ndogo ndogo na kuongeza kuwa mikopo ya wanawake imesaidaia sanan katika jamii kwa kuondoa migogoro  midogo midogo ya kifedha kwa familia .

MWISHO.

NZEGA WAISLAM.

KIKUNDI cha wanaharakati wa wakiislam wilayani nzega mkoani Tabora kinatarajia kuwafungulia mashtaka viongozi wa baraza la waislam tanzaznia wilaya ya hiyo (Bakwata} kwa ubadhifu wa fedha wa zaidi ya shilingi billion 4.8

Fedha hizo ambazo kwa kipindi cha miaka saba hawajawai kusomea taarifa ya mapato na matumizi na bazaar hilo la kiisilamu wa wilaya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa,kiongozi wa kikundi hicho shekhe YUSUF SHABANI.alisema kwamba kwa kipindi chote hicho cha miaka saba hawajui jinsi gani fedha hizo zilivyotumika kwa kipindi cha miaka hiyo saba.

Alisema kwamba wameamua kuwapeleka viongozi hao mahakamani kutoka na baadhi ya viongozi hao kuhujumu miradi ya waislam.

Shabani alisema kwamba fedha hizo zilitokana na michango ya waislam waliochangia michango kwa ajili ya mahabara ya shule ya sekondari ya BADRI kiasi cha shilingi milioni 645.1,ambapo mahabara yenywe bado hajaisha na fedha hazijulikani zilipo.

Alisema licha ya michango ya shule lakini ia fedha za zahanati ya bakwata ziadi ya shilingi bilioni 1.2 hazijulikani zilipo fedha hizo na hazijulikani zilipo.

Kiongozi huyo wa kiislam taarifa ya uendeshaji bwa miradi ambayo bakwata wanapata ni machinjio ya mjinbi nzega,vibanda kuzunguka msikiti wa Ijumaa na ule wa majengo,mnada katika eneo la nzega mjini .

Nyingine ni nyumba,majengo na viwanja vya wakfu,sadaka za Ijumaa na mwezi wa ramadhani,na nyakati nyingine wanaamua kufadhili kusaidia ,zahanati ya bakwata na shule ya sekondari ya badri.

Mwisho

No comments:

Post a Comment