Saturday, August 25, 2012

MADEREVA WATAKIWA KUWA NA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI


MADEREVA

Madereva  nchini wametakiwa kuwa wangalifu na kufuata  sheria za barabarani  kikamilifu ili waweze kuokoa maisha  ya wasafiri na kupunguza ongezeko la ajali za barabarani hapa nchini

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, Saveli Maketta, alipokuwa akikabidhi vyeti kwa madereva wa magari na pikipiki waliopatiwa na mafunzo na chuo cha udereva cha Dodoma, ambacho kinatambuliwa na serikali. 

Alisema iwapo kama madereva watafuata sheria na taratibu za usalama barabarani hakuna shaka kwamba ajali zinazoikabili taifa hivi sasa zitapungua na hivyo kusaidia kuokoa maisha ya watu  wanaokuwa safarini. 

Alisema udereva usiozingatia nidhamu na sheria umekuwa chanzo kikubwa cha ajali za barabarani hapa nchini ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaasa vijana walioingia katika fani hiyo kuwa makini na kuepukana na tabia ya kuleta mzaha wawapo barabarani. 

Mkuu huyo wa wilaya ya Kaliua, alikabidhi vyeti vya udereva kwa  vijana 154 katika wilaya hiyo, ambao walifundishwa na mkufunzi wa udereva anayetambuliwa na chuo cha usafirishaji cha Taifa  (NIT) Marijani Majani. 

Mwenyekiti wa chama cha madereva nchini (TDA) mkoa wa Tabora, Ali Kitenge, aliishukuru serikali kutokana na kuweka program za mafunzo kwa madereva hali ambayo alisema itasaidia uwepo wa umakini kwa madereva wenye sifa zinazotakiwa kuendesha magari na hivyo kupunguza ajali za barabarani.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment