Thursday, August 23, 2012


NA LUCAS RAPHAEL,TABORA

HABARI ZA MKOA WA TABORA

HISA   IGUNGA.

MWENYEKITI wa bodi ya mamlaka ya maji wilaya ya Igunga Costa Olomi ,mkuu wa wilaya ya Igunga Elibaiki Kingu na Sharifa Said,  wameteuliwa kuwa walezi  wa wa jumuiya  ya hisa na  maendeleo  wilaya ya Igunga,  ili wavilee  vikundi vya hisa  kwa lengo la kufikisha maendeleo kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akiwaapisha walezi hao,  mkuu wa wilaya ya Igunga Elibariki Kingu akifunga mkutano mkuu wa jamuiya hiyo aliwataka viongozi hao kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuhakikisha Igunga inasonga mbele.

Alisema kwamba maendeleo ya wanaigunga yatajengwa na wana Igunga mweyewe  kwa maaana hiyo watu wa wilaya ya hiyo wanatakiwa kufanya kazi kwa biidi ili kujiletea maendelo yao wenyewe katika nyanja mbalimbal za kiuchumi.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba anataka wilaya ya Igunga  iwe mfano wa wilaya nyingine mkoani Tabora,  katika kuimarisha kilimo cha chakula na biashara na kuwezesha wakulima kulima na kupata ziada licha ya wilaya hiyo kuwa na uchache wa mvua .

Hata hivyo baada ya Jumuiya hiyo kupata walezi  Costa Olomi alikubalki kuwatumikia wananchi hao,  ili kufanikisha maendeleo ya wananchi hao kwa nguvu zote .

Alisema kwamba amekuwa mlezi wa kikundi hicho  toka mwaka 2007 kwa kuvikusanya vikundi mbalimbali kutoka kikundi kimoja hadi kufikia vikundi 260 vyenye watu 7000 na bado kwa imani hiyo jumuiya hiyo kuona mchango wake ameamua mteue rasmi kuwa mlezi wa kikundi hicho.

 Sharifa  Said alisema kwamba amefurahishwa  kukufanya kazi kwa karibu na mkuu wa wilaya hiyo  kwani  anonekana ni mchapa kazi na mtu mwenye mkakati wa kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya ya Igunga .

MWISHO.


MATREKTA.


Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora inatoa matrekta 12 yenye thamani ya shilingi milioni 450 kwa kata 12 za wilaya ya hiyo kwa ajili ya kusaidia kukua kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara na hatimaye kukuza kipato cha wakulima.

Mkuu wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Elibariki Kingu, aliwataka wakulima kuhakikisha kwamba wanayatumia vizuri matrekta hayo kwa lengo la kuinua uzalishaji na hivyo kuwa na uhakika wa kipato.

Aliwataka wakulima kuongeza ukubwa wa mashamba yao na kuhakikisha kuwa wanayatumia matrekta hayo kwa lengo la kupambana na umasikini kwa kufanyakazi kama watumwa  tena bila ya kuchoka kwa ajili ya manufaa ya familia zao.

Alisema wakumbuke kuwa matrekta hayo yanayotarajiwa kununuliwa na Halmashauri hiyo hayatolewi kama zawadi bali ni mkopo na hivyo watatakiwa kuurejesha mara baada ya kuanza kuuza mazao yao kulingana na mkataba.

Alisema ofisi ya mkuu wa wilaya itaingia nao mkataba kwa lengo la kuhakikisha kuwa vikundi hivyo vya ujasiliamali vinaimarika na vinapata uwezo wa kurejesha mikopo hiyo kulingana na mkataba baina yake na Halmashauri ya wilaya hiyo.

Kwa upande wa  wafanyabiashara wadogo wadogo   waliopo kwenye mji wa Igunga, Mkuu wa wilaya aliwataka wajiunge pamoja na kuchagua uongozi wao ili waonane na viongozi wao na kisha kuandaa utaratibu wa vikundi hivyo kupatiwa mikopo.

Alisema lengo la serikali na halmashauri ya wilaya ya Igunga ni kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara  bila ya kuwasahau wafugaji kuboresha hali zao za maisha kwa kujenga nyumba nzuri za kuishi  na kusomesha watoto.

Mwisho.


Camartec.



Wakulima mkoani Tabora wamekishukuru kituo cha zana za kilimo nchini na ufundi vijijini (CAMARTEC) kutokana na kuonyesha vifaa vya kisasa vyenye kukidhi mahitaji halisi ya matumizi ya zana hizo katika maeneo ya vijijini.

Wakulima hao walitoa shukrani hizo walipotembelea banda la  maonyesho  la CAMARTEC  katika viwanja vya Nane nane vilivyopo kwenye eneo la Ipuli mjini Tabora, ambapo walijionea zana mbali mbali za kilimo zinazotumia teknolojia ya kisasa.

Mkulima  wa Tumbaku na Mahindi mkoani Tabora,  Shaaban Ntahondi, alifurahishwa sana na mashine ya kisasa ya kupuchukua mahindi  ambayo imetengenezwa na CAMARTEC ambapo kwa mujibu wa wataalam wa kituo hicho inauwezo wa kupuchukua gunia tano za mahindi kwa saa.

Alisema mashine hiyo itawasaidia wakulima wengi  kuepukana na matumizi ya kupiga mahindi, ambapo licha ya kutumia idadi kubwa ya watu lakini bado imekuwa haina ufanisi wa kutosha na gharama za kuwalisha watumishi bado ni kubwa.

Alisema pamoja na teknolojia hiyo pia mtambo wa kuchemsha maji kwa kutumia umeme wa jua pia itawasaidia wakulima kuachana na matumizi ya kuni ambazo alisema zimekuwa zikileta madhara makubwa kwa binadamu na viumbe hai kutokana na kumaliza miti.

Mkulima mwingine  Hassan Wakasuvi, alifurahishwa na teknolojia ya matrekta yaliyotengenezwa na CAMARTEC ambayo licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kulima pia yamekuwa yakitumia majembe tofauti tofauti kwa ajili ya kulima, kupanda, kuvuna na kuchambua mazao kwa uhakika.

Alisema kwa ubunifu kama huu tunaweza kumkomboa mkulima wa Tanzania, akaondokana na kilimo cha jembe la mkono ambacho hakina tija na kuweza kujikomboa na kuzalisha mazao mengi zaidi hivyo kuweza kuondokana na njaa.

Aliwataka wakulima wawe wanatembelea manesha ya nane nane kila mwaka kwani yanafaida kubwa  kwao kwa kuona na kupata nafasi ya kuitumia teknolojia mpya zinazozalishwa na wataalam ambazo alisema zitasaidia kuwaondoa katika hali duni.

Katika maonesho hayo CAMARTEC ilioonyesha bidhaa mbali mbali za zana za kilimo ambazo zimebuniwa na kutengenezwa na wataalam wake,  kama mashine ya kukamua mafuta, majiko ya biogas, Matrekta, majembe ya kilimo cha wanyama kazi, majiko banifu na sanifu ya mkaa, Mashine ya kumenya karanga, mashine ya mashine ya kukamua mbegu za mafuta na kadhalika.

Afisa  Masoko wa CAMARTEC Lambart Rwebangira na Meneja wa CAMARTEC tawi la Nzega, mkoani Tabora, Mkoko Yassin  walisema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikibuni zana mbali mbali kwa kutumia teknolojia rahisi ambayo itawasaidia wakulima kuboresha maisha yao na kulisaidia  Taifa kuondokana na tatizo la njaa na ukosefu wa fedha za kigeni kwa kuuza mazao yao nje  ya nchi.


Mwisho.

No comments:

Post a Comment