Thursday, August 23, 2012

Na Lucas Raphael,Tabora

Mwenyekiti.

Baraza la madiwani la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora, limemchagua diwani wa kata ya Ilolangulu katika wilaya hiyo, Said Shaaban Ntahondi,  kuwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mwaka 2015 utakapofanyika uchaguzi mkuu nchini.

Katika kikao chake kilichofanyika makao makuu ya wilaya hiyo mji mdogo wa Isikizya na kuhudhuriwa na madiwani wote 29 wa halmashauri hiyo,  madiwani hao walimchagua diwani Said Shaaban Ntahondi, kuiongoza halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu
.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Uyui, Doroth Rwiza, alisema Ntahondi amepata kura 29 kati ya kura 29 zilizopigwa na hivyo kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo.

Diwani Ntahondi, amechaguliwa kushika nafasi hiyo kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mashaka Kalyuwa, aliyeuwawa kwa kupigwa risasi na majambazi nyumbani kwake Ipuli mjini Tabora, Mwanzoni mwa Mwaka huu.

Aidha Kikao hicho kwa kauli moja kilimchagua diwani wa Igalula, Seleman Kapalu kuwa makamo mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja, kapalu alipata kura 29 kati ya kura 29 zilizopigwa na madiwani wa halmashauri hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Said Ntahondi, alisema kuwa atajitahidi kuiongoza halmashauri hiyo kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na kwamba anachohitaji ni ushirikiano kutoka kwa madiwani na watumishi.
Alisema kwamba bila ushirikiano kati ya wataalam na madiwani kazi kwake itakuiwa ni ngumu kwanio umajo na mashikamano utakuwa ni ndogo ,hivyo rai yake kubwa ni kupata ushirikiano kutoka sehemu zote mbili na tatu kwa viongozi kuwatumikia wananchi kwa nguvu na kasi.
Ntahodi kabla ya kupata nafasi hiyo alikuwa ni makamo mwenyekiti wa halmashauri hiyo na mara baada ya kufariki mwenyekiti wake aliongoza halmashauri hiyo kwa kipindi cha miezi 4.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment