Friday, April 25, 2014

MKUU WA MAJESHI AFUTWA KAZI SUDAN KUSINI


Generali James Hoth Mai amefutwa kazi na Salva Kiir ingawa Rais huyo hajatoa sababu ya hatua yake
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa majeshi yake.
Amri iliyotolewa na Rais kupitia kwa televisheni, ilisema kuwa Generali James Hoth Mai ataondolewa katika wadhifa wake mara moja.
Hata hivyo Rais Kirr hakutoa sababu ya kumfuta kazi generali huyo.
Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na vurugu tangu mwezi Disemba.
Wiki jana waasi waliuteka mji ulio na utajiri mkubwa wa mafuta Bentiu.
Mbali na hayo, umoja wa mataifa ulitoa ripoti iliyohusisha wapiganaji waasi na mauaji ya kikabila.
Na pia imekosoa serikali kwa kutoa taarifa za kupotosha kuhusu mauaji ya halaiki yaliyofanyika mjini Bentiu punde waasi walipouteka mji huo. Mamia wanaaminika kuuawa.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini,Michael Lueth, hakuwa mkweli alipowaambia wandishi wa habari kuwa wakazi waliokuwa wanatafuta hifadhi katika makao ya Umoja wa Mataifa walizuiwa kuingia katika hifadhi hiyo.
Baada ya waasi kuuteka mji wa Bentiu waliwalenga mamia ya raia wasio na hatia na ambao walikuwa wametafuta hifadhi ndani ya msikiti, kanisa na hospitali na kuwaua kwa misingi ya ukabila
Hata hivyo waasi wanaomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais Riek Machar wamekanusha madai ya UN kuwa walihusika na mauaji ya mamia ya raia wasio na hatia huku vituo vya redio katika mji huo vikitumiwa kueneza chuki.

No comments:

Post a Comment