Tuesday, April 15, 2014

WAKULIMA WATAKIWA KUPANDA MITI

 kimarekani.

NA LUCAS RAPHAEL,TABORA

MWENYEKITI wa chama cha msingi WETCU Mkoa wa Tabora, Hassani Wakasuvi amewataka wakulima wa tumbaku wahakikishe wanakuwa na miti mingi yakutosha kwa ajili ya kukaushia tumbaku yao.

Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 21 wa Chama Kikuu cha wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi,WETCU Ltd ,alisema Wakulima wengi hawajaitikia kikamilifu wito wa kupanda Miti.
.

Mahitaji ya miti kwa ajili ya kukaushia Tumbaku ni makubwa na kwamba kama hali haitadhibitiwa ni hatari kwani jangwa litaweza kupatikana.

Wakulima wengi wa tumbaku Mkoa wa TABORA hawana miti ya kutosha kwa ajili ya kukaushia Tumbaku.


Takwimu kuhusu kupandwa kwa Miti mingi lakini kiuhalisia hali ni tofauti kwani miti mingi haikuwi kutokana na sababu mbalimbali.

Wakasuvi ambaye pia Ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora,ametaka Wakulima wa tumbaku kuhakikisha wanakuwa na Miti ya kutosha kwa ajili ya kukaushia Tumbaku yao.

Kwa upande wao wanachama wa WETCU Ltd,wametaka Elimu kuhusu umuhimu wa upandaji miti na utunzaji Mazingira itolewe kwa Wakulima.

Wamebainisha kwamba Elimu ni muhimu ili mazingira yaweze kutunzwa kwa faida ya Wakulima wa sasa na Wakulima wanaokuja.

mwisho

No comments:

Post a Comment