Sunday, April 27, 2014

UKAWA WAMJIBU RAIS KIKWETE


ukawa5 eeb08
Na Hudugu Ng'amilo
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) warudi bungeni akidai hawana sababu ya kwenda kushitaki kwa wananchi kwa sababu watawacheka na kuwasikitikia, umoja huo umemjibu wakisema wapo tayari kuchekwa.

Akihutubia vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) juzi, siku moja kabla ya sherehe za miaka 50 ya muungano, Rais Kikwete alisema kuwa huko nje wanakotaka kwenda UKAWA siko na siku yake sio sasa, hivyo akawaomba wasipoteze fursa hiyo muhimu ya kutoa mawazo yao bungeni ili yafanyiwe kazi.

Alisema wananchi hawahusiki wala hawana namna ya kuwasaidia kwani mengi ya hayo yanayowakasirisha ni matatizo waliyoyazusha wao.

Mwenyekiti wa UKAWA, Freeman Mbowe, aliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa
kama Kikwete anafikiri kwamba watarudi bungeni kwenye mijadala ya dharau, ubaguzi na matusi inayofanywa na wajumbe wa CCM, basi hajui chimbuko la tatizo.

"Kadiri anavyoendelea kuliacha Bunge liendelee na mijadala ya kibaguzi na matusi, taifa linazidi kupasuka na washauri wake hawamwelezi tatizo hilo," alisema.

Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alisema kuwa Rais Kikwete asipokuwa makini atalitumbukiza taifa kwenye machafuko ingawa yeye anafanya utani kwa kuipasua nchi na kushangilia kauli za kibaguzi, kejeli na matusi zinazotolewa na baadhi ya wajumbe wa CCM.

"Rais na wasaidizi wake inaelekea hawajasikiliza hata kauli zinazotolewa na viongozi wa dini kuhusu rasimu ya Warioba, atuache twende kwa wananchi, wao ndio wataamua. Tumevumilia kwa kiwango fulani, lakini itafika mahali uvumilivu utaisha, kwani hatuwezi kuendelea kuzuiliwa kufanya mikutano na jeshi la polisi wakati mikutano ya CCM inafanyika kote nchini kutuchafua," alisema Mbowe.
 

CCM KIMEPANGA MKAKATI WA KUENGUA WATAKA URAIS WANAUME


migiro ec14d
Na Hudugu Ng'amilo
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepanga mkakati mpya wa kuengua wataka urais wanaume kwa kuingiza hisia za kijinsia kama walivyofanya kumdhibiti aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta, alipotaka kugombea tena nafasi hiyo mwaka 2010.

Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wameliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa mkakati huo unalenga zaidi kumng'oa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ambaye anaonekana tishio kwa wenzake wanaotajwa kutaka urais.
Kwa mkakati huo, kundi la wana CCM walio karibu na Rais Jakaya Kikwete, wameanza kuzungumzia jinsi ya kumpitisha Dk. Asha-Rose Migiro agombee urais katika uchaguzi mkuu ujao 2015.

Kisingizio wanachotumia katika kampeni yao ya siri, ni kusaka kura za wanawake.

Katika mkakati huo, wanamwandaa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, kuwa Waziri Mkuu. Tayari Membe ameshatangaza kuwa hatagombea ubunge mwaka 2015.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Membe ndiye alikuwa akipigiwa chapuo zaidi miongoni mwa makada wa CCM ili kurithi mikoba ya Rais Kikwete, lakini kutokana na uhusiano wa kifamilia uliopo baina ya wawili hao, sasa ameshawishiwa kuwa atakuwa waziri mkuu endapo Dk. Migiro atashinda.

Wiki hii, gazeti dada la Tanzania Daima Jumatano liliripoti mkakati wa kumzima Lowassa asigombee urais, ambao unaendeshwa na mtoto wa kigogo akishirikiana na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Dk. Migiro ambaye kwa sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria, na pia Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Nje wa CCM, tayari ameanza kuzungushwa mikoani ili kumjengea uwezo na uzoefu wa kisiasa.

Miongoni mwa wana CCM wanaotajwa kuutaka urais 2015 mbali na Lowassa na Membe, ni Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano), Stephen Wasira, William Ngeleja na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.

"Ukiwalinganisha Membe na Lowassa kwa nguvu na umaarufu ndani ya CCM, hata vigogo wengine wanaotajwa kuutaka urais, utaona hakuna wa kumshinda Lowassa, sasa ndani ya chama wameamua kumchezea rafu.

"Kwa vile ana mtandao mrefu ndani ya CCM, wanafahamu wakikata jina lake itakuwa balaa, hivyo wameona waibuke na hoja ya zamu ya wanawake kama walivyomzima Samuel Sitta asigombee uspika wakampa Anne Makinda," alisema mtoa habari wetu.

Chanzo hicho kinaongeza kuwa mlengwa ni mtoto wa kigogo ambaye anaendesha mkakati wa kumchafua Lowassa ili 2025 ndiye awe mgombea urais baada ya Dk. Migiro kumaliza uongozi wake endapo atachaguliwa kwa vipindi viwili.

Pamoja na mkakati huo, kundi la Membe limeshauriwa kuendelea na harakati za kujiimarisha ili kuhadaa makundi mengine ndani ya chama yaamini kwamba naye ni miongoni mwa watakaochukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais.

Hata hivyo, wakati CCM ikiendesha mkakati huo dhidi ya Dk. Migiro ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, baadhi ya wasomi wamemchambua mwanamama huyo wakisema hana uwezo huo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, alisema kuwa Dk. Migiro haonekani kubadilika licha ya kuwa na elimu kubwa.

"Nilimtembelea ofisini kwake akiwa UN kama Naibu Katibu Mkuu, nilikuwa na kazi za kitaifa kabisa kwa masuala yaliyoshirikisha mabalozi wa Ulaya, lakini aliponiona aliniuliza kwanini sitaki kurejea CCM.

"Huyu hawezi hata kubaini hapa tunazungumzia masuala ya kitaifa au kimataifa, yeye akili yake inawaza CCM tu kila wakati, hajaonyesha kutofautisha u-CCM wake na taaluma ili aweze kusaidia katika nyanja za kitaifa na kimataifa," alisema.

Dk. Slaa aliongeza kuwa aliposikia kuwa Dk. Migiro ndiye aliyeandaa rasimu ya kwanza na ya pili ya katiba kwa upande CCM ambazo zinaleta shida kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba zikikinzana na rasimu ya Tume ya Jaji Warioba, amedhihirisha kabisa udhaifu wake.

"Ukiangalia rekodi zake akiwa UN, huwezi ukaona matokeo yoyote, ndiyo maana Ban Ki moon hakutaka tena asaini mkataba kwa awamu nyingine kwani hakuwa na msaada kwake," alisema Dk. Slaa.

Dk. Azavery Lwaitama ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bukoba ambaye alisema kuwa Dk. Migiro sio mtu mwenye umaarufu wowote ambao unaweza kumfanya amweke katika orodha ya watu wanaoweza kuwa viongozi wa nchi hii.

"Aliteuliwa kuwa Waziri wa Jamii, Jinsia na Watoto, akafanya kazi kipindi kifupi na baadaye akafanywa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati wa awamu ya Rais Kikwete.

"Kutokana na kunong'onezana kati ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon na Rais Kikwete, Dk. Migiro aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na baadaye kwa utaratibu huo huo wa kunong'onezana akarejeshwa tena nchini," alisema.

Dk. Lwaitama aliongeza kuwa vyombo vya habari vya nje viliandika vizuri kuhusu uwezo wa Dk. Migiro wakati akiwa Umoja wa Mataifa, lakini Watanzania hawakujishughulisha kuangalia yaliyoandikwa.

"Nilitarajia kuwa yeye atakuwa na mawazo tofauti katika mjadala wa rasimu iliyopo bungeni, lakini amerudi kwa wana CCM wenzake, anafikiri kama wao, analeta ushabiki wa makundi ya kisiasa, kwa utaratibu huo hawezi kuwa kiongozi anayefaa," alisema.

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) ambaye ni mwanafunzi wa Dk. Migiro, alisema haoni dalili au uwezo wowote wa yeye kuwa kiongozi katika wadhifa huo mkubwa wa urais.

"Huyu hajawahi kushiriki uchaguzi wowote akashinda, ukiwemo hata ubunge, isipokuwa nafasi za kuteuliwa ambazo hupewa na marais.

"Angalia kwa mfano katika Bunge hili la katiba ametoa mchango gani wa kukumbukwa na wananchi licha ya kuchangia na kubaki katika Bunge linalotoa matusi na kuacha kujadili rasimu?" alisema Lissu.

RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO

CCM WILAYA YA TABORA MJINI WAADHIMISHA MIAKA 50 YA MUUNGANO KWA VITENDO!!!

Mjumbe wa kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tabora Bw.Emmanuel Mwakasaka akibeba udongo kwa ajili ya kuwasogezea mafundi katika ujenzi wa ofisi za chama hicho kata ya Kitete ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.
Baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Tabora ambao walishiriki shughuli za ujenzi wa ofisi za CCM kata ya Kitete
Katibu wa siasa na uenezi wa CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Rashid Ramadhani au maarufu Kamanda Tolu

DIWANI LUZILA ASHIRIKIANA NA WANANCHI WA KATA YAKE KUCHIMBA MITARO KWA AJILI YA HUDUMA YA MAJI SAFI


Diwani wa Kata ya Tambukareli Bw.Salumu Luzila akishirikiana na wananchi wa kata hiyo mtaa wa Nkonkole kuchimba mtaro wa kuweka bomba la maji safi kwa ajili ya wananchi wa eneo hilo ambapo Mamlaka ya Maji Safi Tabora mjini wamelazimika kuweka huduma hiyo ya maji kwa wakazi hao.

Friday, April 25, 2014

MKUU WA MAJESHI AFUTWA KAZI SUDAN KUSINI


Generali James Hoth Mai amefutwa kazi na Salva Kiir ingawa Rais huyo hajatoa sababu ya hatua yake
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa majeshi yake.
Amri iliyotolewa na Rais kupitia kwa televisheni, ilisema kuwa Generali James Hoth Mai ataondolewa katika wadhifa wake mara moja.
Hata hivyo Rais Kirr hakutoa sababu ya kumfuta kazi generali huyo.
Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na vurugu tangu mwezi Disemba.
Wiki jana waasi waliuteka mji ulio na utajiri mkubwa wa mafuta Bentiu.
Mbali na hayo, umoja wa mataifa ulitoa ripoti iliyohusisha wapiganaji waasi na mauaji ya kikabila.
Na pia imekosoa serikali kwa kutoa taarifa za kupotosha kuhusu mauaji ya halaiki yaliyofanyika mjini Bentiu punde waasi walipouteka mji huo. Mamia wanaaminika kuuawa.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini,Michael Lueth, hakuwa mkweli alipowaambia wandishi wa habari kuwa wakazi waliokuwa wanatafuta hifadhi katika makao ya Umoja wa Mataifa walizuiwa kuingia katika hifadhi hiyo.
Baada ya waasi kuuteka mji wa Bentiu waliwalenga mamia ya raia wasio na hatia na ambao walikuwa wametafuta hifadhi ndani ya msikiti, kanisa na hospitali na kuwaua kwa misingi ya ukabila
Hata hivyo waasi wanaomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais Riek Machar wamekanusha madai ya UN kuwa walihusika na mauaji ya mamia ya raia wasio na hatia huku vituo vya redio katika mji huo vikitumiwa kueneza chuki.

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA HOSPITALI KUBWA NA YA KISASA YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI KISASA KIJIJINI MLOGANZILA

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chung IL wakikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 24 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini leo April 24, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chungh IL wakiweka udongo kwa pamoja wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, April 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chung IL na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, April 24, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mkasi Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Mhe John Mnyika ili na yeye akate utepe na viongozi wengine kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila mkoa wa Pwani leo April 24, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika sherehe za kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila mkoa wa Pwani leo April 2014. 
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Balozi wa Korea nchini Mhe Chung IL wakiwa mbele ya mchoro wa mfano wa Hospitali ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini leo April 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akifurahi na msanii Mrisho Mpoto baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini leo April 2014. leo April 2014. PICHA NA IKULU

UNHWA YA KOREA KUSINI KUISAIDIA NIMR KATIKA UGUNDUZI WA DAWA KWA KUTUMIA MIMEA

 Na Father Kidevu Blog, Dar es Salaam

Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu Tanzania (NIMR), imesaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya UNHWA ya Jamhuri ya Korea ambapo kampuni hiyo itaisaidia NIMR teknolojia mpya ya kufanya ugunduzi wa dawa za binadamu kwa kutumia mimea.

Makubaliano hayo yamesainiwa jijini Dar es salaam pembezoni mwa kongamano la 28 la kisayansi la NIMR, ambapo mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo Dk. Mwele Malecela amesema hatua hiyo ni muhimu katika shughuli za utafiti wa afya nchini na maendeleo ya taasisi kwa ujumla.

Dk. Mwele amesema teknolojia hiyo itaongeza uwezo wa kiwanda cha taasisi cha kutengeneza dawa kwa kutumia mimea kilichopo eneo la Mabibo External jijini Dar es salaam na kwamba itawezesha taasisi kujikita zaidi katika utengenezaji wa dawa za saratani mbalimbali pamoja na za kusaidia udhibiti wa virusi vya ukimwi.

Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo ya NHWA bw. YOUNG WOO JIN amesema kampuni yake imefikia hatua hiyo kutokana na mchango wa NIMR katika masuala ya tafiti na ugunduzi wa dawa ambapo ameahidi kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika kiteknolojia
ili kuiongezea uwezo.

KWA MUJIBU WA JARIDA LA PEOPLE, HUYU NDIYE MWANAMKE MZURI ZAIDI DUNIANI MWAKA 2014

Lupita Nyong'o mwanamke mrembo zaidi duniani mwaka 2014.



  Jarida la People limemtangaza Mkenya Lupita Nyong’o kama mwanamuke mrembo zaidi duniani mwaka 2014.

Lupita ambaye alishinda tuzo ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu '12 years a slave,' yuko kwenye ukurasa wa juu zaidi wa makala ya wiki hii ya jarida hilo.

Katika orodha yake ya wanawake 50 warembo duniani,Lupita amewapiku waigizaji maarufu akiwemo Kerry Washington, ambaye pia alishiriki katika filamu hiyo na mwanamuziki Pink ambao walikuwa katika nafasi ya 10 na 5 mtawalia.

Jarida la People limemtaja Lupita kuwa mwanamke mrembo

Stacy Kiebler ambaye alisifika sana kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji nyota George Clooney, alishikilia nafasi ya nane.
Hatua ya Jarida la People ambalo huchapishwa kila wiki nchini Marekani na kusomwa na karibu watu milioni 40, kumkubali Lupita kama mwanamke mrembo duniani, ni kama tuzo kivyake kwa muigizaji huyo ambaye amegonga vichwa vya habari nchini Marekani tangu kushinda

Mtandao wa People.com, unasema kuwa muigizaji huyo alifurahia sana kutajwa na jarida hilo kama mwanamke mrembo hasa kwa sababu wasichana kama yeye watapata kuwa na matumaini ya kufanikiwa maishani kama yeye.

"Nimefurahi sana na hii ni fursa kuwafanya wasichana wengine wajihisi kuwa wana uwezo wa kufiia chochote maishani mwao.

MAZISHI YA DC CHANG'A YALIVYOKUWA

Utaratibu  wa mazishi  ukiwekwa
DC Mwamoto kulia na DC Warioba  wakiwa msibani hapo
DC Mwamoto akiweka  sahii kitabu cha maombolezo .
Spika Makinda akitoa  mkono wa pole kwa wafiwa
Spika Makinda  kulia akimpa pole waziri Hawa Ghasia
Spika Makinda  akiwapa pore  wafiwa
Spika  wa bunge Anne Makinda akiwa amepiga magoti  kuwapa  pole  wafiwa katika msiba wa aliyekuwa DC wa kalambo Moshi Chang'a leo mjini Iringa
Waombolezaji  wakiwa katika msiba  huo  .
Spika wa bunge Anne makinda akisaini kitabu cha maombolezo ya DC Chang'a .
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia akisaini kitabu  cha maombolezoo ya  aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Mussa Chang'a leo nyumbani kwake mjini Iringa kabla ya mazishi  yaliyofanyika makaburi ya Mtwivila 
Spika Anne Makinda akiteta  jambo na waziri Hawa Ghasia  .
Mwanahabari  Eliasa Ally Chang'a( kulia)  ambae ni ndugu na DC Chang'a akiwa na waombolezaji  wengine Msafiri Mtandi kushoto na Said kalinga katikati
Mwenyekiti  wa CCM Kilolo Sety Mwamoto kulia  akiwa na mdau
mfanyabiashara  mkubwa Iringa Pilly MOhamed  akisainia kitabu cha maombolezo
Mkuu wa mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma akisaini kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya kalambo Rukwa marehemu Moshi  Chang'a wanaoshuhudia ni mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita kushoto na mkuu wa wilaya ya  Iringa Dr Leticia Warioba katikati ,hapa ni nyumbani kwa marehemu eneo la Kihesa mjini Iringa
RC Mbeya Bw kandoro  akiwapa pole  wafiwa
Mke wa mkuu wa mkoa wa Mbeya akisaini kitambu cha maombolezo ya Dc Chang'a
Mkuu wa mkoa wa Mbeya akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo
Waombolezaji  na ndugu  wakiwa katika viwanja vya maombolezo  
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza akitoa  salam za chama
Kiponza akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro  
Mbunge Msigwa akiwa na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akitoa  salama zake na za Chadema pamoja na ubani wa TSh 100,000
Vijana  wa  CCM wakiweka mambo  sawa
Wakuu wa  wilaya  mbali mbali nchini  wakiwa  wameubeba mwili wa DC mwenzao Moshi Chang'a .
Mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamwoto  kulia akishirikiana na mkuu wa wilaya ya Mwanza  kukunja bendera  iliyotumika kufunika mwili wa DC Chang'a
Kada wa CCM Iringa mjini Frederick Mwakalebela akishiriki msiba  huo
Wakuu wa wilaya na wananchi  Iringa  wakiwa  wamebeba mwili wa Dc Chang'a mjini Iringa .
Mwili wa DC Chang'a ukipelekwa msikiti wa Mwanchang'a Kihesa
Waombolezaji  wakielekea msikitini  .
Umati wa wananchi  wakielekea makaburi ya Mtwivila  
Msafara  wa kutoka nyumbani kwa DC Chang'a kwenda msikitini
msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete katika masuala ya siasa Ikulu Rajab Luhwavi kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita kulia  wakati wakielekea kumzika Dc Chang'a leo mjini Iringa .