Friday, December 20, 2013

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA ATEMBELEA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI TABORA


Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Bw.Alfred Luanda akizungumza na baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu ya Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Tabora TBPC,kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw.Theonas Liwa,anayefuata ni Katibu wa chama hicho Bw.William Mahimbo na Vivian Pyuza ambaye ni Mwekahazina mkuu wa TBPC.Mkurugenzi huyo alitembelea ofisi ya chama hicho na kushauri mipango ya maendeleo ya TBPC ikiwa ni pamoja na kuwataka viongozi hao kuomba kiwanja kwa ajili ya kujenga ofisi kubwa.   
Mkurugenzi huyo wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Bw.Alfred Luanda ilikuwa ni mara yake ya kwanza kutembelea ofisi ya klabu ya Waandishi wa habari Tabora ambapo uongozi wa ulimweleza changamoto kadhaa zinazoikabili klabu hiyo yenye wanachama wasiopungua 32.

No comments:

Post a Comment