Friday, December 20, 2013

WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 120



Na Lucas Rphael,Nzega


MAHAKAMA ya Hakim mkazi wilayani Nzega Mkoani Tabora imewahukumu watu wa wa 4 kwenda jela miaka 120 kutokana na kukutwa ha hatia ya kufanya unyan`ganyi kwa kutumia silaha.

Waliotiwa hatiwa hatiani na mahakama hiyo ya  hakimu mkazi  ni  ,Joseph Manala(38),Emmanuel machibya(20)Juma Lutalamula(30)Juma msabato(42).

Akisoma hukumu hiyo hakim mkazi wilaya ya nzega, Silvester Kainda watuhumiwa wa nne (4)  wametiwa hatiani kwa kosa la kuvamia kwa kutumia siraha na kupewa hukumu ya miaka 120 huku kila mmoja akitumikia miaka 30 gerezani.

Alisema kwamba vitendo vya unyan`ganyi kwa kutumia silaha vimekuwa vikiongezeka kila siku jamboo ambalo linatishia amani ya watanzania hivyo dhahabu kali ndio lilio sahii kwa watu waina hii.

Alisema kwamba hiyo iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo ya kupara mali zawatu ambao wametafuta kwa jasho lao na wengine kuchukua mali hizo kama zao..

Hakimu kainda aliiambia mahakama hiyo kwamba ushidia uliotolewa mahakani hapo umeonyesha bila shaka na kufanya mahakamni iweze kuwatia hatiani washitakiwa hao kwani nikweli walitenda kosa hilo  .

Hata hivyo mahakama hiyo imewaachia huru watuhumiwa wawili baada ya kuonekana kutokuwa na hatia katika shitaka hilo kuwa ni Peter Steven (30) pamoja na Ramadhani Juma (19).

Awali mwendesha mashitaka wa Jeshi la polis wilaya Melito Ukongoji aliiambia mahakama  hiyo kuwa mnamo April 5 mwaka huu katika cha  kijiji cha Itanana kata ya Bukene walikuiba Duka la Joakim John mkazi wa kijiji hicho kisha na kumjeruhi vibaya mwili wake.


Mwendesha  akisoma shitaka hilo alisema kuwa watuhumiwa hao waliiba fedha zaidi ya laki saba na kufanya uhalibifu mkubwa wa mali ikiwa na kumjeruhi Joakim John huku wakitumia siraha aina Gobole na mapanga.

Kabla ya kutolewa kwa hukum hiyo mwendesha mashitaka Melito aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa watuhumiwa hao kutokana na kukithiri kwa matukio hayo ili iwe fundisho kwa watu kama hao.

Wakati wa kujitetea watuhumiwa hao waliiomba mahakama hiyo itoe hukum ndogo kutokana na baadhi yao kuwa ni waathirika wa Virusi vya ukimwi huku wengine wakikabiliwa na majukum ya kifamilia.





Mwisho.

No comments:

Post a Comment