Tuesday, December 31, 2013

MWAKASAKA AIPIGA TAFU TIMU YA NETBALL TABORA,AKABIDHI ZAIDI YA SHILINGI MILIONI MBILI


Mlezi wa Chama cha Netball mkoa wa Tabora Emmanuel Adamson Mwakasaka akikabidhi zaidi ya shilingi milioni mbili kwa Katibu wa Chama hicho ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu ya Netball ya mkoa wa Tabora ambayo inashiriki michuano ya Taifa ya mchezo huo,fedha hizo ambazo zitasaidia nauli ya kwenda jijijni Dar-es-salaam ambako mashindano hayo yanafanyika.
Mkuu wa wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuiaga timu hiyo katika hotel ya Wilca mjini Tabora ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka wachezaji wa timu hiyo kujiamini wakiwa mchezoni hatua ambayo itasaidia kuwapatia ushindi ambao utarejesha heshima ya mkoa wa Tabora kutokana na mchezo huo.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Netball ya mkoa wa Tabora.

Mwakasaka ambaye pia ni mdau wa michezo mkoani Tabora alitumia fursa hiyo kuwaahidi wanamichezo hao kuwapa ushirikiano katika kuendeleza mchezo wa Netball huku akiwataka wachezaji kumuunga mkono kwa kufanya vizuri katika michuano ya Taifa wanayoshiriki  sasa.
Mdau wa mchezo wa Netball Hamisi Msoga naye alipata fursa ya kumkabidhi Mwakasaka mchango wa shiriki 50000/= kwa ajili ya kusaidia timu hiyo ya Netball.
Kiongozi wa timu ya Netball ya mkoa wa Tabora ambaye alikuwa akimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Tabora Suleimani Kumchaya wakati akitoa hotuba ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment