Saturday, December 21, 2013

WATOTO WANAOHISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI WAPATIWA MSAADA



  NA LUCAS RAPHAEL TABORA

Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya  Tabora Christian Youth Network imetoa wa  maada wa vifaa vya shule kwa watoto waishio katika mazingira hatarishi katika kata za kakola, Uyui na Gongoni katika wilaya ya tabora .

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo ,Adriano Kalisti, alisema kuwa kwa ufadhili wa shirika la kimarekani liitwalo SAVE AFRICAN’S CHILDREN .
Alisema kwamba shirika hilo limekuwa litoa huduma za vifaa vya shule kwa watoto waishio katika mazingira hatarishi kama vile madaftari na kalamu.


Alisema kwamba kutoa msaada wa kisaikolojia kwa watoto waishio na virusi vya ukimwi na walioathiriwa wapato 75 na  kuanzisha clubs maalumu zinazowakutanisha watoto hao kila mwezi kwa ajili ya kupata elimu ya afya, kupata huduma za kisaikolojia kwa kucheza michezo mbalimbali.

Alisema kuwamba  changamoto mbalimbali wanazopitia kulingana na hali zao pamoja na kupata chakula cha pamoja chenye lishe kwa ajili ya ujengaji wa afya zao.


Kalist alisema  kuwa wanakusudia kusaidia jumla ya watoto 500 katika kipindi cha miaka mitatu yaani 2013-2016  katika maeneo ya kuwajengea walezi/wazazi wao kiuchumi, Afya, elimu, ulinzi na kutoa msaada wa kisaikolojia.


Alisema mnamo mwezi January 2013 CYN inajarajiwa kuendesha program maalumu ya kukusanya watoto zaidi ya 300 ili luwashirikisha, upendo, Furaha kwa kula chakula cha pamoja, kucheza michezo mbalimbali, kuwezesha watoto kutoa hisia zao kwa jamii juu ya matatizo wanayopitia.


Alisema kuwa wanatarajia kuzindua kampeni maalumu ijulikanayo kwa jina la “ HURUMIA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI KATIKA ENEO LAKO, BEBA MZIGO” Kampeni hii imelenga kuhamasisha jamii kuwa na moyo wa dhati/ mzigo wa kusaidia watoto waishio katika mazingira katarishi katika maeneo waishio bila kutegemea wahisani.


Alisema kwamba shirika la Christian Youth Network inakaribisha wadau wengine kama vile makampuni na watu binafsi katika kudhamini shughuli hii muhimu inayotarajiwa kufanyika Mwaka mpya 2014 katika tarehe za mwanzoni.

Mwisho

No comments:

Post a Comment