Friday, December 20, 2013

MSANII WA UGANDA ZIGGY DEE KUACHIA NGOMA MPYA YA KIHISTORIA TABORA "LIVINGSTONE CITY"

Friday, November 29, 2013

Ziggy Dee msanii toka Uganda aliyetamba na Eno Mic akiwa studio za Kapestone-Tabora
Producer EiZeR BiT kwenye mashine
Kushoto: Producer EiZeR BiT, Ziggy Dee na Pro. BK mavinanda.
Wadau wa ukweli kwa pozi
Appson, Ziggy Dee na Stone Wa Kitaa [wa kulia] - wote wasanii
Ziggy Dee na Ma-Producer wake.

Na Lucas Raphael,Tabora.
Ziggy Dee, ambaye ni msanii pekee wa Afrika mashariki na kati  akiwa ni mara yake ya kwanza kuingia katika mkoa wa Tabora na kufanya wimbo unaousifia mkoa huo.
Katika wimbo wake huo aliouita kwa jina LIVINGSTONE CITY msanii huyo nguli wa muziki wa kizazi kipya  amedai kuwa kihistoria katika vitabu vinavyosomwa kwingineko duniani kote, Tabora imekuwa ni sehemu maarufu kama moja ya njia na kituo  cha biashara ya utumwa enzi za ukoloni wa waarabu na waingereza.
Ziggy ambaye ameweka wazi kuwa  na Tabora ikiwa ni moja ya Trade routes maarufu,ambayo mmoja kati ya viongozi wa wakoloni  Dr. David Livingstone alipita na kuweka himaya yake enzi hizo za harakati za kutokomeza biashara ya utumwa  iliyokuwa ikifanywa na dola ya  Waarabu,hatua ambayo inazidi kuimarisha historia ya mkoa wa Tabora na kufanya ni moja ya vivutio vya utalii kwa maliasili za kale zinazotokana na mabaki au masalia ya majengo,njia za watumwa na vitu mbalimbali vya asili ya Mwafrika.

Licha ya historia ya pekee ya mkoa wa Tabora iliyouwekea ramani ya dunia katika masuala ya utalii wa mali za kale, msanii huyu Ziggy amezungumzia kuwa haijalishi kuwa yeye ni  raia wa Uganda lakini akaweka bayana kuwa Afrika ni moja na Waafrika wote ni ndugu wanaostahili kujivunia tunu hiyo ya uwepo wa historia kubwa isiyo na mfano huku akidai kufurahishwa kwake kufika mkoa wa Tabora kwa mara ya kwanza baada ya kupafahamu kupitia  historia zilizoandikwa kwenye vitabu mbalimbali na hatimaye yeye pia kufika kwake atakuwa ameandika historia ya pekee na hasa kuandaa wimbo huo maalumu LIVINGSTONE CITY ambao pia ataufanyia video kabla ya kurejea nyumbani nchini Uganda.

Aidha kazi nzima ya kurekodi wimbo huo  imefanywa katika studio za hapahapa mkoani Tabora ifahamikayo kama KAPESTONE chini ya uongozi wao Ma-Producer  EiZeR BiT na BK (Baraka mavinanda). Ngoma hiyo ina mahadhi ya Raga na inatarajiwa kutambulishwa mapema hivi  karibuni.


No comments:

Post a Comment