Sunday, December 29, 2013

WAATHIRIWA WA MAFURIKO TABORA WAPATA MSAADA WA UNGA WA MAHINDI


Baadhi ya waathiriwa wa mafuriko yaliyotokea hivi katika  kata za Malolo na Chemchem zilizopo manispaa ya Tabora wakisubiri mgawo wa msaada wa Chakula kilichotolewa na Ofisi ya halmashauri ya manispaa ya Tabora kufuatia nyumba zao kukumbwa na mafuriko hayo na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na Chakula na hivyo Serikali kuamua kutoa msaada huo kwa waathiriwa zaidi ya 102. 
Mstahiki Meya wa manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij akikabidhi msaada wa Chakula kwa diwani wa Kata ya Malolo Bi.Zinduna Kambangwa kwa ajili ya watu waliokubwa na mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mjini hapa ,ambapo makabidhiano hayo yalifanywa mbele ya Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Bw.Suleiman Kumchaya,Mbunge wa jimbo la Tabora mjini Bw.Ismail Rage pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Bw.Alfred Luanda ambapo msaada huo ni tani moja na robo ya unga wa mahindi. 
Baadhi ya Waathiriwa wa mafuriko hayo wakisaidiana kubeba unga ambao ni kilo 25 walizopatiwa kila mmoja.

No comments:

Post a Comment