Sunday, December 30, 2012

taarifa kwa umma:USITISHAJI WA MATANGAZO YA ANALOJIA NA KWENDA KATIKA MFUMO WA DIJITALI

TAARIFA YA MHE. JANUARY Y. MAKAMBA (MB), NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUHUSU USITISHAJI WA MATANGAZO YA ANALOJIA NA KWENDA KATIKA MFUMO WA DIJITALI

Ndugu Wananchi,

Mtakumbuka kuwa hapo tarehe 23 Februari 2012 tuliwatangazia kupitia vyombo vya habari juu ya usitishwaji wa matangazo ya televisheni kwa kutumia teknolojia ya analojia kwenda katika mfumo mpya unaotumia teknolojia ya dijitali.

Napenda kuwaleleza kuwa, maandalizi ya kuzima mitambo ya analojia kuanzia tarehe 31 Desemba 2012 yamekamilika kwa mujibu wa makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo, napenda sasa kutoa taarifa kuwa uzimaji wa mitambo ya analojia utafanyika kwa awamu kama ifuatavyo:-

(1) Dar Es Salaam-31 Desemba, 2012;
(2) Dodoma & Tanga- 31 Januari, 2013;
(3) Mwanza-28 Februari, 2013;
(4) Moshi & Arusha-31 Machi, 2013;

(5) Mbeya-30 Aprili, 2013.
Tumeamua kuanza kuzima mitambo hiyo kwa Jiji la Dar es Salaam kwanza ili kutoa fursa kwa makampuni yenye leseni kusimika mitambo ya utangazaji wa dijitali katika mikoa mingine. Makampuni haya yamejipanga kukamilisha usimikaji wa mitambo hiyo katika mikoa minane katika miezi minane ijayo.

Mitambo ya analojia itakayozimwa kesho ni ile iliyopo Kisarawe na Makongo. Vituo ambavyo siku ya tarehe 1 Januari 2013, vitapaswa kuanza kutangaza matangazo kwa mfumo wa dijitali ni TBC1, ITV, EATV, Channel 10, StarTV, DTV, CapitalTV, TumainiTV, ATN, MlimaniTV, C2C, CTN, CloudsTV na Efatha.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inafanya jitihada za kutosha kuhakikisha kwamba makampuni yenye leseni za kusambaza ving’amuzi yanakuwa na ving’amuzi vya kutosha na vingine vimeagizwa ili kukidhi mahitaji ya baadaye na vile vilivyopo sokoni vina ubora unaokubalika.

Vilevile, Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itahakikisha kwamba zoezi la uhamaji linafanyika bila usumbufu na kero kwa wananchi. Makampuni yanayouza ving’amuzi yameagizwa yaimarishe huduma kwa wateja wakati wa kuuza ving’amuzi na hata baada ya ununuzi iwapo wananchi watakuwa na matatizo na ving’amuzi.

Zoezi hili la uhamaji ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Tutakapokuwa tumekamilisha uhamaji, huduma za mawasiliano na utangazaji zitapanuka na kuwa bora zaidi. Kwa mfano, itawezekana sasa kuangalia televisheni kupitia simu zetu za mikononi. Vilevile, itawezekana, kwa bei nafuu kabisa, kwa mtu mwenye uwezo wa kutengeneza vipindi kukodisha chaneli yake na kutangaza vipindi vyake. Vilevile, bei za mawasiliano na utangazaji zitashuka, na tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwenye mapinduzi ya teknolojia duniani, ambayo nchi yetu haiwezi kubaki nyuma.

Ndugu Wananchi,

Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhamaji huu. Serikali inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa wadau wa sekta ya utangazaji na wananchi kwa ujumla katika kipindi cha uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni ili kufanikisha zoezi la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya teknolojia ya analojia.

Uhamaji huu hautahusu televisheni za wananchi zinazopata matangazo kupitia madishi (nyungo) (satellite) au nyaya (cables). Hivyo, wananchi wanaopata matangazo kupitia DStv, Zuku, na nyinginezo wataendelea kupata matangazo yao kama kawaida.

Ndugu Wananchi

Kama kuna mwananchi yoyote ana kero, malalamiko, swali au anahitaji maelekezo kuhusu uhamaji, awasiliane na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia namba 0784-558270; 0784558271 au barua pepe: malalamiko@tcra.go.tz

Ndugu Wananchi,

Nawashukuru kwa kunisikiliza

TUZO HII NI KWA WADAU WOTE WA FULLSHANGWEBLOG NA KUKARIBISHA MWAKA MPYA 2013


Mkurugenzi wa Fullshangweblog.com Bw. John Bukuku kushoto akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki katika maonyesho ya World Travel Market (WTM)Nchini Uingereza mwezi Oktoba mwaka huu katikati ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utaii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena.
.........................................................

Mwaka huu Fullshangwe imefanikiwa kupata Tuzo ya kutangaza utalii wa ndani wa Tanzania kimataifa mwaka 2011 nchini Uingereza inayoitwa TANZANIA TOURISM BOARD WEB TRAVEL MAGAZINE AWARD 2011, Fullshangweblog.com kupitia kwa mkurugenzi wake Bw. John Bukuku ilipokea tuzo hiyo katika maonesho ya utalii ya kimataifa ya dunia World Travel Market (WTM) yaliyofanyikaneo katika eneo la Exel jijini London nchini Uingereza kuanzaia Oktoba 5 mpaka 8 2012, ambapo Fullshangweblog.com ilikuwa moja ya makampuni yaliyoshiriki katika maonyesho hayo katika kupasha habari.

FULLSHANGWEBLOG.COM inaushukuru uongozi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inayoongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji Dk Aloyce Nzuki, Mkurugenzi wa Masoko Devotha Mdachi , Meneja Masoko Bw. Geofrey Meena na wafanyakazi wote wa bodi hiyo, pamoja na wadau wake wote kwa kutambua mchango wa FULLSHANGWE.BLOG kama web magazine iliofanya kazi nzuri ya kutangaza utalii wa ndani mwaka 2011 na kuitukukia tuzo hiyo, ninawashukuru sana kwani maana ya tuzo hii ni kwamba tunamaliza mwaka 2012 kwa mafanikio.

Kuna baadhi yamambo niliyokumbana nayo katika kazi zangu za kila siku ” Kuna matukio mengi niliwahi kukutana nayo katika shughuli zangu za kutafuta habari mengine yalikuwa ni ya kukatisha tamaa sana, lakini sikukata tamaa niliendelea kukaza buti kadiri mungu alivyonijalia, Lakini mengine yalikuwa ni ya mafanikio yenye kutia moyo.

Katika kazi hii nimekumbana na mambo mengi “Kuna wakati marafiki zangu wa karibu walinikatisha tamaa na kuniuliza kwamba ninafanya nini mbona sieleweki hasa wakati nilipojitambulisha katika mikutano mbalimbali kwamba nawakilisha WWW.FULLSHANGWEBLOG.COM wengi hawakunielewa hata kidogo nini ninachokifanya, hata hivyo niliendelea na juhudi zangu mpaka walipoanza kutambua na kuelewa kwamba nilikuwa nafanya nini”

Siku moja nilisafiri kuelekea nyanda za juu kusini mkoani Iringa nilifika katika wilaya Mufindi Mafinga nilikutana na kisa ambacho pia nilikiripoti kwenye mtandao, kisa hiki kilikuwa hivi.

MAPANDA HOTEL WANASEMA LAPTOP COMPUTER INAKULA UMEME KULIKO PASI NA FRIJI!

Nimeingia katika hoteli hii ya Mapanda Hotel and Guest House mjini Mafinga ili niweze kupata kifungua kinywa lakini pia niweze kufanya kazi zangu kwenye kompyuta yangu ya mkononi, lakini sikupata kifungua kinywa wala kufanya kazi yoyote, Kilichonipoza ni kutumia Kompyuta yangu (Laptop) Meneja wa Hoteli hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alinifuata na kuniambia kwamba siwezi kuendelea kutumia kompyuta yangu kwa kuwa inakula sana umeme ni sawa tu na friji au pasi ya umeme, hivyo ningeweza kumaliza umeme wao wa LUKU, nikajaribu kubembeleza lakini meneja huyo alinikatalia kabisa..

Binafsi sikujali sana wala sikukubaliana na hoja yake manake nilijua kwamba umande na umbumbumbu umewajaa kwenye ubongo wao katika teknolojia ya Kompyuta hivyo kwao wao Kompyuta ya mkononi au Laptop ni sawa usiku wa giza, Ikabidi niondoke hapo lakini bahati nzuri nikapata Internet Cafe inayoitwa 3A Traders Internet Cafe hapo nikafanya kazi yangu vizuri kabisa

Nawatahadharisha ndugu zangu mnataka kuja na kompyuta zenu hapa Mafinga msijisumbue kwenda hapo Mapanda Hotel kwani yanaweza kuwapata yalionipata mimi.

MATUKIO YA KUKUMBUKWA
Kati ya matukio ambayo ni ya kumbukumbu kubwa ni tukio la kuzama kwa September 10, 2011 ambalo mtandao wa Fullshangweblog.com uliripoti kwa ufupi na kuvuta hisia za watembeleaji wengi MELI ya Spice Islander imezama usiku wa kuamkia leo ikiwa safarini kuelekea Pemba ikitokea bandari ya Malindi Unguja.

Meli hiyo inasemekana ilikuwa na abiria wapatao 610 ambapo juhudi za kuokoa majeruhi wa ajali hiyo bado zinaendelea hivi sasa.

Akizungumzia ajali hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi amesema tukio hilo limetokea saa 8:30 za usiku.

Haji Ussi amesema meli hiyo iliondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima, lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubinuka na hatimaye kuzama kabisa.

Lakini pia tukio linguine lililovuta hisia za watembeleaji wengi lilikuwa ni kifo cha Mwigizaji Maarufu nchini Marehemu Steven Kanumba watu wengi walikuwa wakitembelea mtandao ili kupata taarifa mbalimbali juu ya msiba huo.

NINAJISIKIA VIZURI KUWA BLOGGER

Nimekuwa nikifurahia kazi yangu na kuipenda sana kwani katika kazi yangu hii ya kupasha habari imenikutanisha na watu wengi maarufu, wasio maarufu lakini ni muhimu katika jamii na wakati mwingine ninaposafiri katika mikoa mbalimbali na vijiji na nje ya nchi, kitu kikubwa kinachonifurahisha ni matukio halisi ninayokutana nayo, kwani nakutana na habari mabazo zinagusa hisia za wasomaji na watembeleaji wa mtandao na pia zinanifanya kujifunza mambo mengi yanayotokea duniani pia napata habari zaenye uhalisia wa maisha ya mtanzania na matukio yenye kuvuta hisia kwa wasomaji wetu, jambo ambalo linanifanya nijisikie vyema zaidi ninapopata nafasi ya kupiga picha na kuandika habari za kijamii kutoka vijijini katika mikoa mbalimbali na mataifa mbalimbali hii ni kutokana na mvuto wa picha na habari zenyewe lakini pia ninapata changamoto za kimawazo na jinsi ya kujikwamua katika maisha ya kila siku.

SHUKURANI KWA WADAU
Mwisho ninawashukuru wadau wote waliofanikisha hapa kwa njia yoyote ile mafanikio ya mtandao wa FULLSHANGWEBLOG.COMsi kwa juhudi zangu binafsi juhudi binafsi, bali pia ni juhudi za wadau wote ambao tulishirikiana nao na tunaendelea kushirikiana nao kwa moyo wa dhati, ni matumaini yangu kwamba tutaendelea kushirikiana kwa karibu ili tuweze kuendeleza juhudi za kujenga nchini yetu nzuri ya Tanzania na kupasha habari zaidi kadiri tutakavyojaliwa na Mwenyezi Mungu katika mwaka ujao wa 2013

Lakini naomba nitaje baadhi ya taaisisi, mashirika na wadau kadhaa waliotusaidia na wanaendelea kutusaidia kwa kututumia habari na matukio mbalimbali, ninatoa shukurani kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Idara ya Habari Maelezo, Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Kitengo cha habari Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Habari Ofisi ya Makamu wa Rais, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Kitengo cha habari Ofisi ya Bunge, Vitengo vya habari Katika Wizara mbalimbali, Mashirika, Makampuni binafsi, Idara za serikali na wadau mmoja mmoja waliotusaidia kupata habari mbalimbali muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.

Nitakuwa siyo mwingi wa fadhila kama sitawashukuru kaka zangu Muhidin Issa Michuzi na Maggid Mjengwa, kaka zangu walionitangulia kwa umri na kazi ya kublogu ninawashukuru kwa ushauri wo ninaoweza kuuita maalumu pia kwa msaada wao katika kunielekeza mambo mengi juu ya uelewa wa kublogu, ambao nimekuwa nikipewa wakati wote, nashukuru sana kaka zangu naomba tuendelee na moyo huohuo na mungu atatutangulia katika yote, Lakini pia niwashukuru mablogger wenzagu Michuzijunior wa Jiachieblog au Ahmed Michuzi kama anavyojulikana, Mroki Mroki, Zainul Nzige, Carthbert Kajuna, Othman Michuzi, Abdalla Mrisho, Josephat Lukaza na Mwanamke blogger mkongwe Mamaa Shamimu Mwasha wote ninawapenda sana

Mwisho napenda kumshukuru dada yangu, mwandishi wetu na mpiganaji Gladness Mushi wa FULLSHANGWEBLOG.COM mkoani Arusha, ninakushukuru dada yangu kwa kuipigania FULLSHANGWEBLOG na kuitambulisha kwa nguvu mkoani Arusha kutokana na habari nyingi za kijamii ambazo umekuwa ukizituma kutoka huko, tuko pamoja na FULLSHANGWE inakuangalia kwa macho mawili Mungu akubariki sana na uwe na afya njema ili tuendeleze kazi

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe:“Kama Mwenyezi Mungu atampa uhai na afya njema hadi mwaka 2015, Dk Slaa anatosha na Chadema, tutampa fursa nyingine ya kupeperusha bendera ya chama kwenye nafasi ya urais ninataka wanaotumia ugombea Urais kama kete ya kuleta mtafaruku ndani ya Chadema watambue hivyo.”

 

 Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe Akiunguruma Karatu
 Mbunge wa Arumeru Mashariki-CHADEMA,Joshua Nasari akiunguruma Karatu jana mbele ya Umati Mkubwa
Sehemu ya Umati mkubwa wa Wana Chadema Karatu wakiwa kwenye mkutano wa hadhara jana
--
CHAMA  cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),kimetangaza kuwa Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa atapewa fursa ya kuwania nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, mwaka 2015.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza hatua hiyo jana,alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mpira,mjini Karatu mkoani Arusha, huku yeye akijiweka kando kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo,Dk Slaa mwenyewe alipoulizwa iwapo ana nia ya kugombea urais mwaka 2015, alisema: “Kwani mwaka 2010 nilijitangaza mwenyewe?,Iwapo wanachama wa Chadema watanipendekeza, nitafikiria kufanya hivyo.”Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea......>>>>>

MAGHALA YA KUHIFADHIA BIDHAA ZA WAFANYA BIASHARA WA MWANJELWA JIJINI MBEYA YATEKETEA KWA MOTO USIKU

Maghala ya kuhifadhia bidhaa mbali mbali za wafanya biashara wa mwanjelwa Mbeya yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo maghala hayo yapo maeneo ya uwanja wa ndege wa mwanjelwa
Wanausalama wakiwa makini na vibaka ambao walitaka kuvamia eneo hilo la moto kutaka kupora mali kujifanya wanaokoa mali hizo
Hakika kikosi cha zimamoto cha jiji la mbeya wakishirikiana na kikosi cha zimamoto uwanja wa ndege wa songwe walijitahidi kuuzima moto huo ingawa mara kwa mara waliishiwa maji kutokana na uwezo mdogo wa magari hayo kubeba maji ya kuzimia moto
Moja ya gari ya kampuni ya jambo ikiungua moto katika maghala hayo
Moja ya wafanyabiashara hao ambaye anamizigo yake katika maghala hayo akikatazwa na mwanausalama kwamba asiende kuokoa mali zake kwani moto ni mkubwa awaachie kikosi cha zimamoto kifanye kazi yake
Mfayabiashara huyo haamini mcho yake huku akilia akiona bidhaa zake zikiteketea kwamoto
Hakika jeshi la polisi linastahili pongezi kwa kazi kubwa ya kuokoa mali za wafanyabiashara ambao bidhaa zao zilikuwa katika maghala hayo hapa polisi wakiwa wamemshika kibaka aliyetaka kuiba mafuta ya kupikia
Kwakweli ilikuwa hatari kwani vibaka walikuwa wanarusha mawe kwa polisi na kwa baadhi ya magari hapa hili gari ikitoka katika ghala hilo likiwa limevunjwa kioo cha mbele
Baadhi ya wananchi wengi wakiwa katika tukio hilo
Haya si maji bali ni mafuta ya kula ambayo yamemwagika baada ya blastiki kuyeyuka kwa moto
Asubuhi hii moto ndiyo unaishia
Hali halisi baada ya kuungua kwa maghala hayo hili si tope mali ni mafuta ya kula yaani mafuta ya kupikia
Baadhi ya wafanyabiashara wakijaribu kuokota baadhi ya mabaki ya bidhaa zao zilizopona katika moto huo
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Athuman Diwani akiongea na waandishi wa habari leo amesema anawapongeza sana wakazi wa Mbeya hasa wale wa maendeo yanayozunguka maghala yalioteketea kwa mtoto kwa ushirikiano wao kuwezesha kuokoa baadhi ya bidha za wafayabiashara licha ya vijana wachache kutaka kuiba na kutupa mawe askari wake ili wafanye uhalifu wa kupora bidhaa zilizokuwa zinaokolewa hapo mpaka sasa vijana wawili wamekamatwa kwa kutupiaaskari mawe na kuiba bidhaa zilizokuwa zinaokolewa
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda diwani.PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG

Thursday, December 27, 2012

HOJA YA MDAU: UFAHARI WA KWENYE MISIBA UONESHENI KATIKA UGONJWA WA MZEE SMALL


Staa wa Vichekesho na Filamu Bongo, Said Mohamed Ngamba ‘Mzee Small’ akiwa amelazwa hospitali kutokana na maradhi yanayomsumbua.
KWENU mnaohusika na sanaa ya filamu Bongo. Mnajitambua sina haja ya kuwataja mmojammoja kwa majina, nitamaliza ukurasa bure.

Mimi najua mpo poa, mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Binafsi niko poa, naendelea na majukumu yangu ya kila siku ikiwamo hili la kuwaandikia barua.

Barua yangu leo moja kwa moja nailekeza kwa nyinyi wote ambao watu sasa hivi wanawatambua kwa jina la mastaa wa filamu katika soko la Bongo, Bongo Movies.
Kikubwa ni kwamba, natambua mchango mlionao katika kusogeza gurudumu la maendeleo ya nchi. Natambua umuhimu wenu wa kuwatibu watu kisaikolojia kupitia filamu zenu mnazozifanya. 
Hongereni kwa hilo.Katika taaluma yangu ya uandishi wa habari, mara kadhaa nimeshuhudia uwezo wenu katika kufanikisha mambo yanayowahusu, iwe ni sherehe au misiba.
Eeeh, kwenye sherehe basi mnalipuka na kushangweka kwelikweli. Kwenye misiba, mnahakikisha mnamsindikiza mtu anayewahusu kwa hadhi anayostahili.
Hoja hapa ni kwamba, hadhi ile ambayo mnajitutumua hadi kwenye misiba, kwa nini tusioneshe kwa mkongwe wa sanaa nchini, Said Ngamba ‘Mzee Small’? Tunashindwa nini? Mbona pesa zipo? 
Kwa nini tusimsaidie mzee wetu ambaye tunaimani alikuwa chachu ya vijana wengi kuingia kwenye sanaa?
Mzee wetu anasumbulia na ugonjwa wa kupararazi. Anashindwa kufanya shughuli zake za sanaa ambazo ndiyo chanzo cha pato lake la kila siku.
Binafsi nilisikitishwa na kupongeza kitendo cha Rais wa Shirikisho la Filamu nchini TAFF, Saimon Mwakifwamba kuingilia kati na kuanza kutembeza ‘bakuli’ la michango kwa ajili ya kumsaidia mzee huyo.
Nilisikitika kwani sikuona haja ya yeye kuingilia kati suala hilo ambalo naamini lilikuwa chini ya uwezo wenu, mnaweza bwana! Kikubwa ni kipi haswa? Mbona mna ‘mauwezo’, msinifanyie hivyo bwana.
Kwani kuna tatizo gani tukiweka nukta katika starehe hata kwa siku moja, tusipige kilevi siku hiyo halafu tujichangishe fedha za kumpa sapoti mwenzetu kwenye kipindi hiki ambacho anaumwa?
Hakika hili ni dogo, tukiamua tunaweza tena haliwezi kuharibu bajeti zenu hata kidogo.
Ni yule yule,
Mkweli Daima.
Joseph Shaluwa

RAISI WA ZANZIBAR DK SHEIN AKUTANA NA WAJUMBE WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar,Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar,(ZEC) Khatib Mwinyichande,akiongoza ujumbe wa Tume hiyo walipofika Ikulu Mjini Zanzibar,Kumuaga Rais kwa kumaliza muda wa kazi wa Tume hiyo jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar,Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea Ripoti ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar,(ZEC) kutoka kwa Mwenyekiti wake Khatib Mwinyichande,alipoongoza ujumbe wa Tume hiyo walipofika Ikulu Mjini
Zanzibar,Kumuaga Rais kwa kumaliza muda wa kazi wa Tume hiyo
jana.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad:'Mwaka wa 2012 ni mwaka wa historia'

   Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa kufunga mwaka uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti.
Mwakilishi wa Jimbo la MjiMkongwe Zanzibar Ismail Jussa Ladhu (CUF), akiwahutubia wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa kufunga mwaka uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti.
   Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Hamad Massoud Hamad, akiwahutubia wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa kufunga mwaka uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti.
  Wafuasi na wapenzi wa CUF wakiwa katika mkutano wa kufunga mwaka ulioandaliwa na chama hicho katika viwanja vya Kibandamaiti.
  Wafuasi na wapenzi wa CUF wakiwa katika mkutano wa kufunga mwaka ulioandaliwa na chama hicho katika viwanja vya Kibandamaiti.Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
--
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema mwaka 2012 umekuwa na umuhimu wa kipekee katika historia ya kisiasa Tanzania.
Amesema ndani ya mwaka huu unaomalizika Watanzania katika mikoa yote wamepata fursa ya kutoa maoni yao juu ya uundwaji wa katiba mpya ya Tanzania ambayo yatatoa mwelekeo imara wa mustakbali wa nchi.
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akihutubia mkutano maalum wa hadhara wa Chama hicho kwa ajili ya kuuaga mwaka 2012, uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti Zanzibar.

Amesema suala la kuwashirikisha wananchi katika jambo kubwa kama hilo la kuamua juu ya mustakbali wa nchini yao ni la kihistoria, na kutaka maoni ya wananchi wa pande mbili za Muungano yathaminiwe na yaheshimiwe.
 
Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kubariki uundwaji wa katiba mpya ya Tanzania na kuwashirikisha wananchi, suala ambalo lilikosekana katika awamu zilizopita za uongozi.
 
“Nachukua fursa hii kumpongeza sana Rais Kikwete kwa kubariki jambo hili, wakati wa marehemu Mwalimu Nyerere ilionekana kama uhaini kuzungumzia masuala ya Muungano hadharani lakini leo hii kila mwananchi anayo haki ya kuujadili kabisa”,alieleza Maalim Seif na kuongeza kuwa hiyo ni hatua kubwa zaidi ya kisiasa kuwahi kufikiwa Tanzania.
 
Ameuombea mwaka mpya wa 2013 uwe wa neema ambao utaisababishia Zanzibar kusonga mbele katika kufikia malengo yake iliyojipangia.
 
Maalim Seif amewashuku wananchi wa Zanzibar kwa kuonyesha mshikamano wakati wa utoaji wa maoni, na kwamba umoja wa Wazanzibari ndio utakaopelekea kupatikana kwa Zanzibar yenye mamlaka kamili ndani na nje ya Zanzibar.
 
Kwa upande wake Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Hamad Massoud Hamad amesema chama chake kinajipanga kwa ajili ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Amewaomba wananchi kuendelea kukiunga mkono chama hicho ili kiweze kutatua kero ya ukosefu wa ajira unaowakabili vijana wengi wa Zanzibar.
 
“Vijana wengi wa Zanzibar bado hawana ajira, vijana hawa wamesoma wengine hadi vyuo vikuu na wazee wao wametumia fedha nyingi kuwasomesha lakini wapi, ajira imeota mbawa”,alisema Hamad Massoud.
 
Nae Mwakilishi wa Jimbo la Mjimkongwe Ismail Jussa Ladhu, amesewa Wazanzibar wameitumia vyema fursa yao ya kutoa maoni, tofauti na ilivyoelezwa na baadhi ya wajumbe wa Tume wa kukusanya maoni.
 
Amefahamisha kuwa maoni waliyoyatoa Wazanzibari ni sahihi na wala hawakupoteza fursa hiyo kama ilivyodaiwa, ikizingatiwa kuwa suala la msingi kwa Zanzibar ndani ya Muungano ni “Muungano wenyewe” kwa vile Zanzibar ina katiba yake ambayo imeweka wazi juu ya masuala yote yanayohusu nchi ya Zanzibar.

 Na 
Hassan Hamad 
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar

BILAL MUSLIM MISION YAWEZEHA WATU 90 KUWEZA KUONA WILAYA YA RUANGWA


 Mkuu wa wilaya ya Ruangwa,Agness Hokororo akiwasalimia baadhi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa macho bila malipo kwa udhamini wa Bilal Muslim Mission wilayani humo
 Mbunge wa Jimbo la Ruangwa ambae pia ni Naibu waziri wa Tamisemi,Kassim Majaliwa akiwa na Bi Somoe Omary alipomtembelea katika hospital ya wilaya ya Ruangwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa macho na kuweza kuona baada ya kutoona kwa miaka 10
 Bi Somoe Omary akifurahi baada ya kufanyiwa upasuaji na kuweza kuona baada ya kutoona kwa miaka 10
 Bango la matangazo
Mbunge wa Ruangwa akiwa pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ,Reubern Mfune wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wagonjwa waliotibiwa na kuweza kuona.
Picha zote na Abdulaziz Video

TBL YAFANIKISHA UPANDAJI MITI 2600 MWANZA


 Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry  Mongi, akipanda mti  wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Steven Kilindo,  akifukia udongo kwenye shimo alilopanda mti wakati wa kampeni ya  upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki..Wanaoshuhudia katikati ni Meneja Ubora wa kampuni hiyo, Caroline Muhonoli na nyuma ya Kilindo ni  Diwani wa Kata ya Mkuyunim, Lugo Fashen.TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600.
 Meneja wa TBL Mwanza, Richmondx Raymond akipanda mti katika uzinduzi wa mradi  wa upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, uliofanywa na kampuni  hiyo kwa kupanda miti 2600 kando kando ya barabara za Balewa, Kenyatta,  machemba na shule za sekondari Nyamaganana na Nyegezi na Kiwanda cha Bia cha kampuni hiyo.

SIKU YA WACHAGA YAFANA SANA MJINI MOSHI



chagga day ilivyopambwa ndani ya zumbaland mjini moshi.


boda 2 boda wakiwajibika jukwani shoo ya chagga day moshi ndani ya zumbaland.


ommy dimpoz akiimba na washabiki chagga day moshi.


ommy dimpoz akimuimbisha mtoto shoo ya chagga day ndani ya zumbaland.


thecla mgaya 'aisha' wa mambo hayo alikuwemo ndani ay nyumba akifurahia chagga day pale zumbaland moshi.
baadhi ya wanamuziki wa serengeti band ya arusha kabla ya kutumbuiza tamasha la chagga day moshi ukumbi wa kisasa wa zumbaland.
mtoto akichorwa katika mashamsham ya chagga day ukumbini Zumba Land.
mkurugenzi uhuru museum akitoa historia ya kabila la wachagga.

Tamasha kubwa la kihistoria lililopewa jina la Chagga Day Cultural Festival 2012 - Moshi lilifanyika kwenye ukumbi wa ZUMBA LAND katika manispaa ya Moshi siku ya Jumamosi tarehe 22/12/2012 kuanzia saa sita mchana mpaka saa sita usiku na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji huo huku baadhi wakioongozana na familia zao.

Tamasha hilo lililotawaliwa na shangwe za mara kwa mara kutoka kwa wakazi wa mji wa Moshi waliofurika kwenye viwanja hivyo maarufu kwa michezo ya watoto, liliandaliwa na kampuni ya Myway Entertainment ya jijini Dar chini ya Mkurugenzi wake Paul Mganga na kudhaminiwa na kampuni ya bia (TBL) kupitia bia ya Safari Lager na kampuni ya vinywaji baridi (SBC) kupitia kinywaji chake murua cha Pepsi.