NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
SHIRIKA la lilisilokuwa la kiserikali la JIDA Tanzania mkoani Tabora limeanza kutoa
mbinu kwa wananchi kuhusu ufuatiliaji wa mkakati wa Serikali wa kukuza uchumi
na kupunguza umaskini MKUKUTA awali ya pili.
Akizungumza na ukurasa huu Afisa uhusiano wa JIDA
,John Pinini amesema kwamba shirika lake kwa ufadhiri wa Foundation For Civil
Society wameamua kutoa elimu hiyo ili jamii iweze kutambua umuhimu wa kushiriki
kikamilifu katika shughuli za kijamii na kujiletea maendeleo miongoni mwao.
Pinini alisema kuwa lengo kuu la kutoa hiyo ni
kuongeza uelewa na ujuzi kwa jamii kuhusu MKUKUTA pia hiyo na kutoa sauti zaidi
ili mwananchi waweze kushiriki kwa juhudi na maarifa katika kazi za mandeleo
kwenye maeneo wanayoishi.
Aidha alisema kwamba dhumuni lingine la kutoa
mafunzo hayo ni kutaka wananchi waelewe mbinu za kufuatilia utekelezaji wa
MKUKUTA na kwamba ni kutaka kuona fursa ya majadiliano ya kisera ukuaji wa uchumi
na kupunguza umaskini kwa mwananchi wa kawaida inakuwepo.
Hata hivyo Pinini amebainisha yakwamba ushiriki
mdogo wa wananchi pamoja na wadau, katika kupanga mipango ya maendeleo
umepelekea Serikali kushindwa kufikia malengo yake ya mkakati wa kukuza uchumi
na kupunguza umasiini kwa wananchi wake.
Ameeleza kuwa iwapo wananchi hao watafahamu
umuhimu wa kufanyakazi kwa badii na maarifa ikiwa ni pamoja na kuzalisha
chakula cha kutosha uchumi kwa jamii unaweza kukua na kuwa na maisha bora
kuliko ilivyo sasa.
Alisema kuwa ili kufanikisha malengo ya Milienia
ya MKUKUTA awamu ya pili ni lazima kila mwanajamii awe mkulima, mfanyakazi,
biashara, wavuvi, viongozi wa Serikali, mashirika ya hiyari, na wadau wa
maendeleo washiriki kwa vitendo kusimamia utekelezaji na kutathimini maendeleo
ya MKUKUTA.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment