Na. Aron Msigwa - MAELEZO.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Saidi Meck Sadiki amewaomba wakazi wa jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa
wingi kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika
zitakazofanyika katika Uwanja wa Uhuru jiji Dar es salaam.
Maadhimisho hayo yameanzimishishwa
mfumo wa aina yake na kuhudhuriwa na viongozi wengi wa ndani na nje ya nchi.
Akitoa ufafanuzi wa kukamilika
kwa maandalizi ya sherehe hizo leo jijini Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki
amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali
kutoka ndani na nje ya nchi na mwaka huu mkoa wa Dar es salaam umepewa heshima
ya kuandaa sherehe za kutimiza miaka 51 ya uhuru.
Amesema katika kipindi cha
miaka 51 ya uhuru Tanzania imepata mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali
za uchumi, ulinzi na usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa.
Amefafanua kuwa mgeni rasmi
katika maadhimisho hayo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.Jakaya Kikwete na kuongeza kuwa yataongozwa na kauli mbiu isemayo
Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu.
Aidha amefafanua kuwa sherehe
za mwaka huu zitahudhuriwa na ugeni wa marais kutoka Jumuiya ya Nchi za Kusini
mwa Afrika (SADC) na kupambwa na gwaride maalum lililoandaliwa na vikosi vya
ulinzi na usalama vya Tanzania , halaiki maalum, vikundi mbalimbali vya
burudani vya ngoma za asili vya hapa Tanzania hususani kutoka maeneo ya
Ukerewe, Dodoma na Zanzibar.
Vikundi vingine vitakavyopamba
sherehe hizo ni kundi la Taifa la sanaa kutoka nchini Rwanda (Rwanda National
Ballet).
No comments:
Post a Comment