Wanachama wa UWF (Unity of Women
Friends) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza matembezi
yao hisani ya kilometa tano kwa ajili ya kuchangisha fedha za
kuwasomesha watoto wa kike wa shule ya Tandika na Tabata sekondari ambao
wanaishi kwenye mazingira magumu na wengi wao wanatoka kwenye familia
duni,matembezi hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki huku mgeni rasmi akiwa
ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la HakiElimu,Bi.Elizabeth Missokia
(wa tatu kutoka kulia)..
Wanachama wa UWF (Unity of Women
Friends) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule
ya Tandika na Tabata sekondari
Mgeni rasmi,Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la HakiElimu,Bi.Elizabeth Missokia akizungumza machache wakati wa hafla fupi ya kuchangisha
fedha za kuwasomesha watoto wa kike wa shule ya Tandika na Tabata
sekondari ambao wanaishi kwenye mazingira magumu na wengi wao wanatoka
kwenye familia duni,Bi Elizabeth kupitia shirika hilo la HakiElimu
waliahidi kutoa shilingi milioni tatu ikiwa sehemu ya mchango wao
kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu.
Mwenyekiti wa UWF
(Unity of Women Friends),Esther Wakati akifafanua madhumuni/lengo la
matembezi hayo ya hisani kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa
wengine,Easther alisema kuwa lengo la matembezi hayo ni kuchangisha
shilingi milioni 80,ambazo zitasaidia kusomesha wanafunzi 100,Tandika
wanafunzi 50 na Tabata wanafuzi 50 kwa kipindi cha miaka 4.
Mweka hazina wa UWF
(Unity of Women Friends),Bi.Mwate Mwadinda akitoa makusanyo
yaliyopatikana kwenye matembezi hayo ya hisani ya Kilometa tano,Mwate
alisema kuwa hafla yao imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni
kumi na laki mbili,hiyo ikiwa ni hatua ya awali ya muendelezo wa
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa kike ambao wanaishi kwenye mazingira magumu na wengi wao wanatoka kwenye familia duni
Meneja Mradi wa SOMKI (Somesha
Mtoto wa Kike),Bi Jane Magembe akizungumza machache mbele mgeni rasmi na
wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo fupi,kuhusiana
mradi/mfuko wa SOMKI unatumika kuwasomesha watoto wa kike waishio katika
mazingira magumu,Mradi huo uko chini ya UWF.
Baadhi ya wanafunzi wanaosomeshwa
na mfuko wa SOMKI,kutoka kulia ni Khadija Hassan Chizenga anaesoma
kidato cha nne shule ya Sekomdari Kunduchi Girls High School pamoja na
Ummilkhery Abdallah anaesoma kidato cha sita shule ya sekondari Benjamin
William Mkapa high school.
Wanachama wa UWF wakifurahi jambo.
Baadhi ya wageni waalikwa
waliofika kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika ndani ya Police Oficcers
Mess,Oysterbay,jijini Dar mwishoni mwa wiki.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,aitwae Vumi akiimba kwa hisia mbele ya wageni waalikwa.
Pichani juu na chini ni wanachama
wa UWF wakiwa na mgeni rasmi sambamba na wageni waalikwa wakiwa kwenye
matembezi ya hisani ya kilometa tano,yakiwa na lengo ya kuchangisha
shilingi milioni 80,ambazo zitasaidia kusomesha wanafunzi 100,Tandika
wanafunzi 50 na Tabata wanafuzi 50 kwa kipindi cha miaka 4.Matembezi
hayo yalidhaminiwa na taasisi ya Foundation for Civil Society,kampuni ya
Clouds Media gROUP,Securix,ITRATECH LTD,Prime Time Promotions,Cool Blue
pamoja na Equip Davith Kahwa.
No comments:
Post a Comment