Tuesday, December 4, 2012

NAFASI ZA UFADHILI WA MASOMO YA SEKONDARI KWA YATIMA WA KIKE


  NAFASI ZA UFADHILI WA MASOMO YA SEKONDARI KWA YATIMA WA KIKE

RafikiElimu  FOUNDATION  ni  Taasisi  isiyokuwa  ya  kiserikali  inayo  jishughulisha  na  Maendeleo  ya  jamii. Taasisi  inapenda  kutangaza  nafasi  za  ufadhili  wa  masomo  ya  sekondari  kwa  waombaji  wenye  sifa  zifuatazo  :

1. Awe    yatima  wa  jinsia  ya  kike  au  awe  masichana  anayeishi  katika  mazingira  magumu.

2.Awe  raia  wa  Tanzania.

3. Awe  anajiandaa  kujiunga  na  masomo  ya  kidato  cha  kwanza  kuanzia  Januari  2013. AU 

4. Awe  anajiandaa  kujiunga  na  masomo  ya  kidato  cha  tano   katika  mwaka  wa  masomo 2013/14.

5. Awe   ni  mwanafunzi  ambaye  tayari  anasoma sekondari   lakini   anashindwa/ ama  ameshindwa  kuendelea  na  masomo  yake  kutokana  na  kufiwa  na  wazazi ama  walezi wake.

*  N.B  : Ufadhili  wa  masomo  kwa  kidato  cha  tano  na  sita   utatolewa  kwa  wanao  taka  kuchukua  masomo  nya  michepuo  ya  ARTS.

Tuma  barua  yako  ya  maombi  ya  ufadhili  wa  masomo  kwenda  kwa :

MKURUGENZI  MTENDAJI,
RAFIKIELIMU   FOUNDATION,
S.L.P  35967,
DAR  ES  SALAAM.

*   Katika  barua  yako  ambatanisha  barua  ya  serikali  ya  mtaa  unaoishi, cheti  chako  cha  kuzaliwa ama  Hati  ya  Kiapo " AFFIDAVIT " , picha  zako nne  za  rangi, pamoja  na  vielelezo  vingine  vinavyo  thibitisha  kwamba  wewe  ni  yatima.

* Maombi  yako  yatufikie  kabla  ya  tarehe   07  JANUARY 2013.

*  Maombi  yanaweza  kutumwa  na  msimamizi  wa  mwanafunzi  husika  kwa  niaba  yake.

Kwa  maelezo  zaidi  tembelea   www. rafikielimu. blogspot.com

No comments:

Post a Comment