Mipira ya Kondom.
KONTENA
lililosheheni kondomu za kiume kutoka nchini India imekamatwa na
kuzuiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kubainika kuwa
hazifai kwa matumizi ya binadamu.
Maofisa
wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamelazimika kufanya msako mkali
kwenye baadhi ya maduka ya dawa jijini Dar es Salaam baada ya kubainika
kwamba tayari kondomu hizo zipo sokoni.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
TBS, Leandri Kinabo alizitaja kondomu hizo kuwa ni aina ya Melt Me zenye
thamani ya Sh222.1 milioni zilizokamatwa tangu Oktoba 23 mwaka huu na
kuzuiliwa bandarini hapo kwa taratibu zaidi za kisheria.
“Jambo
lililotushtua ni kwamba zimebainika kwamba zipo madukani, tukajaribu
kufuatilia tena bandarini tukifikiri kuwa huenda zimetolewa kinyemela
licha ya kuzuiliwa ili ziteketezwe au zirejeshwe nchini India kwa
gharama zao wahusika.
Tulipokwenda
bandarini tukabaini kwamba bado zipo katika hali ile ile, kumbe
zimeingizwa nchini kwa njia ya panya, kwa kweli ni mbovu na ndiyo maana
tumelazimika kuwajulisha wanahabari ili muwape taarifa wananchi wawe
makini,” alisema Kinabo.
Alifafanua
zaidi kwamba kondomu hizo ni mbovu kwani zimebainika kuwa na vitundu,
pia zinapasuka haraka, hazina kabisa viwango vya ubora wa bidhaa
unaotakiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO).
Kinabo
alisema kuwa TBS bado wanaendelea kufanya mawasiliano na kampuni
iliyotengeneza kondomu hizo, lakini kwenye kasha lake inaonyesha kuwa
inaingizwa nchini na kampuni ya Fair Deal Exim ya Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment