Tuesday, December 18, 2012

DC SIKONGE ANUSURU CHAMA CHA MSINGI KUSAMBARATIKA


Na Hastin Liumba,Sikonge

SERIKALI wilayani Sikonge,mkoa wa Tabora,imenusuru chama cha msingi

Mgambo kilichopo kata ya Kitunda,kusambaratika kufuatia wanachama
kutoridhishwa na uongozi wao wakidai ni wabadhirifu na wazembe.

Mkuu wa wilaya ya Sikonge Hanifa Selengu,ndiye aliwasihi wakulima wa

zao la tumbaku kuachana na mawazo ya kuvunja chama hicho chenye
wakulima zaidi ya 349 kugomea kulima zao la tumbaku.

Akizungumza na wanachama wa chama hicho katika viwanja vya shule ya

sekondari Kiwele,Selengu aliwataka wakulima hao kutofikiwa hatua hiyo
kwani ushirika una manufaa makubwa kwao.

“Tafadhalini nawaomba msikifie maamuzi ya kuvunja chama chenu kwani

eneo lolote lile ushirika una manufaa makubwa na kama kuna badhi ya
viongozi wabadhirifu serikali imefika na matatizo yenu
yatashughulikiwa hapa bila uonevu.

Hatua hiyo ya wakulima na kumuomba mkuu wa wilaya kuja kuwasikiliza

kilio chao,inatokana na kutoridhishwa na utendaji wa viongozi wao,huku
mtuhumiwa mkubwa ni mtunza stoo wa chama hicho,Stanford Meshack,
ambaye anadaiwa kudanganya kuwa mbolea ya pembejeo iliyosalia ghalani
imeoza wakati siyo kweli.

Aidha ukali wa wakulima hao unatokana na taarifa ya ukaguzi toka ofisi

ya ushirika wilaya ya Sikonge ya mwezi septemba 30,2012 hadi mwezi
agosti 2012 ikiwemo matumizi ya mkopo na pembejeo toka benki ya CRDB.

Katika ukaguzi huo imeonyesha kuwa daftari la mklima katika madeni yao

halikuandaliwa na taarifa hizo kupotea,huku madeni ya wakulima
kuhusiana na mkopo wa pembejeo nao hawakufuatiliwa.

Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosomwa mbele ya mkuu wa wilaya

chama kilikopa benki dola 329,427 huku marejesho ya mkopo ni dola
364,985.11 pamoja na riba,huku chama kikizalisha kilo 273,879 sawa na
mauzo dola 501,277.94 huku faida ya chama ikibaki kuwa dola
136,291.94.

Aidha taarifa ya ukaguzi toka ofisi ya mrajisi halmashauri Sikonge

imeonyesha pia kuwa malipo kwa mkulima yalistahili kuwa dola 197,398
hali ambayo inaonyesha kuwa kuna upungufu wa dola 61,106.05.

Taarifa hiyo pia inaonyesha kuwepo upotevu wa pembejeo wenye thamani

ya dola 7,848.19 yalisababishwa na mtunza stoo Stanford Meshack
aliyedai pembejeo kadhaa zilioza,madeni yaliyolazwa ni dola 12,805.47
kwa mwaka 2012,pembejeo zilizobaki kwenye mkopo ni dola 50,495.03.

Hatua hiyo ilimfanya mkuu wa wilaya ya Sikonge Hanifa Selengu,kutamka

kuwa mtunza stoo Stanford Mshack akamatwe na kufikishwa mahakamani,na
wakulima wote waliolaza madeni yao walipe mara moja,huku akiwaonya
wakulima baadhi wanaotorosha tumbaku kuwa dawa yao iko jikoni
inachemka na atawashughulikia.

Mkuu huyo wa wilaya aliagiza pia baadhi ya amdeni ya kizembe bodi ya

chama hicho itawajibika kuyalipa,huku mengine karani wa chama hicho
atalipa na mengine wanachama walipe.

Aidha umauzi wa mkuu wa wilaya ulipelekea wakulima hao kadhaa kusimama

na kumhakikishia mkuu wa wilaya kuwa mgogoro huo umeisha na wanarudi
mashambani kuzalisha mzao yote ya chakula na biashara ikiwemo tumbaku.

No comments:

Post a Comment