UHALIFU WAWATESA WAKAZI WA ISEVYA MANISPAA YA TABORA
Mama
mmoja mkazi wa Isevya akitoa machozi kwa uchungu na kushindwa kutoa
maelezo jinsi alivyofanyiwa vitendo vya kiharifu na baadhi ya vijana wa
Isevya ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo wizi na ujambazi,ilikuwa
ni mkutano wa pamoja kati ya wakazi wa kata hiyo uongozi wa Jeshi la
Polisi mkoa wa Tabora.
Mkuu
wa upelelezi makosa ya jinai mkoa wa Tabora RCO BUKOMBE akizungumza na
wananchi wa kata ya Isevya manispaa ya Tabora katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kituo kidogo cha Polisi Isevya.
Mkuu
wa kituo kikubwa cha Polisi Tabora anayeshughulikia kitengo cha Polisi
Jamii Joseph Matui akitoa maelezo ya dhana shirikishi jamii kwa wakazi
wa kata ya Isevya manispaa ya Tabora baada ya kuitishwa kwa kikao
ambacho wakazi hao walikuwa wakifikisha malalamiko yao kuhusu mgambo
wanaofanya kazi katika kituo hicho Kidogo cha Polisi Isevya,ambapo
imeelezwa kuwa mgambo hao wamekuwa wakiomba na kupokea rushwa kwa
wananchi na kusababisha kero kubwa.
No comments:
Post a Comment