NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
Wananchi wa wilaya
ya Nzega mkoani Tabora wametakiwa kulima mazao yanayohimili ukame
kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha kutotosheleza kwa mazao
mengine ambayo hulimwa kila mwaka hasa mahindi .
Wito huo umetolewa na
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya Amosi Kanuda katika kikao cha
wanachama wa chama hicho kilichofanyika katika Jimbo la Bukene wilayani hapa.
Kanuda alisema wananchi
wahamasishwe kulima mazao ya yanayohimili ukame kutokana na mvua za msimu huu
kutotosheleza zaidi kwa mazao mengine ambayo wamezoea kulimwa na wananchi wengi
wa wilaya hiyo.
Alisema baadhi ya wananchi
hulima mazao kwa mazoea ,hali ambayo hugeuka kuwa ombaomba kila mwaka wa
chakula cha njaa kutokana na kutopokea ushauri huo wa kitaalamu kutokana na
eneo hili la wilaya ya nzega .
Akitoa maelekezo kwa
wanachama hao kuwa mazao wanayo takiwa kulimwa na wananchi wa wilaya hiyo ni
pamoja na mtama,viazi vitam,mihogo pamoja na mazao ya kibiashara ambayo yanayo
himili ukame ikiwa na pamba na Alizeti.
Mwenyekiti akiendelea
kutoa wito wake alisema wananchi wakipokea kauli hiyo na kulima mazao hayo
hawatakuwa ombamba wa chakula kila mwaka kutokana na kupata mazao mengi ikiwa
na kupata mazao mengi ya kibiashara kwani mazao hayo yote yanahimili ukame.
Aliongeza kuwa chama hicho
kitaishauri serikali ya wilaya kuhakikisha mbegu za mtama na mbegu za mazao
mengine zinaletwa mapema ili wananchi waendelee na kilimo hicho waendane na
kalenda ya kilimo.
Mwenyekiti huyo aliwataka
wananchi kutunza chakula walicho nacho kwa matumizi mazuri ambayo
amchokitawasaidi kuwafikisha msimu wa mavuno utakao kuja.
’’wananchi na wanachama
chama hakijawakataza kulima mahindi mpunga hapana lakini nguvu kubwa wekene
kwenye mazao yanayo himili ukame kwani mvua hizi hazitoshi,tusilime kwa mazoea kama tulivyo zoea tunataka tuondokane na kuwa
ombaomba’’alisema mwenyekiti huyo.
Kwaupande wake katibu wa
chama hicho wilaya, Kajoro Vyohoroka aliwataka wananchi kuitikia wito huo kwa
pamoja bila kujali itikadi ya vyama vya siasa,dini wala kabila kutokana na
suala hilo
kumgusa kila mtu.
Alisema endapo wananchi
wataitikia wito huo wataondokana na kuwa ombaomba wakila mwaka wa chakula cha
msaada nabadala yake itakuwa historia kwa wananchi hao.
Kwa upande wa wananchama
hao na wananchi waliobahatika kuzungumza na mara baada ya kikoa hicho
walisema kuwa serikali ipeleke haraka mbegu hizo mtama ikiwa na mihogo ili
wananchi waweze kulima mapema zao hilo
.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment