Wednesday, December 5, 2012

VIWANDA JIJINI KUANGALIA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA KUTUNZA MAZINGIRA.


Mkurugenzi wa Tahmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo akitoa taarifa fupi kwa waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC ambapo amesema Wizara imetoa agizo la kufanya ziara katika Viwanda vilivyopo eneo la Mikocheni na fukwe za hoteli zilizoko katika bahari ya Hindi maeneo ya Manispaa ya Kinondoni kujionea changamoto za uchafuzi wa mazingira katika maeneo hayo ambayo huleta athari kwa jamii kwa ujumla. Katikati ni Mkuu wa Msafara Naibu Waziri wa Nchi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga na kulia ni Mkemia Mkuu wa Mazingira katika Ofisi hiyo Bi. Rogathe Kisanga.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya kufanikisha udhibiti wa Mazingira Mhandisi Dr. Robert Ntakamulenga kutoka NEMC akitoa maelezo kwa Naibu Waziri ambapo amesema NEMC imetoa agizo kwa wamiliki wa Viwanda kuhakikisha wanafunga mitambo maalum yakusafisha maji taka yatokanayo na bidhaa wanazozitengeneza hasa zinazotumia rangi kabla ya kuyamwaga katika mifumo ya maji machafu ili kupunguza athari za uharibu wa mazingira.
Naibu Waziri wa Nchi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akizngumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza ziara ya kukagua Viwanda na Mahoteli yaliyopo maeneo ya fukwe za bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam ambapo amewataka Watanzania kuzijua na kuzifwata sheria za Mazingira ikiwemo sheria ya mwaka 2004 namba 20 inayowataka watu kutunza mazingira yanayowazunguka.
Mwanasheria wa NEMC Bw. Mwanchane Heche akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri kuhusiana na hatua zinazopaswa kuchukuliwa kisheria kwa watu wanaochafua mazingira wakiwemo wanaomwaga maji machafu yenye kemikali zinazoharibu Mazingira kutoka viwandani wakati wa ziara ya kukagua Mto Mlalakuwa uliopo maeneo ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Huu ndio Mto Mlalakuwa Kawe Darajani unavyoonekana ambapo maji yake yanaonyesha kuchafuliwa na maji taka yatokayo viwandani.
Mkurugenzi wa Tahmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo akifafanua jambo kwa Mh. Charles Kitwanga wakati wa ziara hiyo sambamba na jopo la waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali.
Eneo la Mto Mbezi lenye mgogoro kufuatia kuzuia mtiririko wa maji ya Mto huo ambalo limenunuliwa na mtu Binafsi anayefahamika kwa jina la Robert Mgishwagwe ambaye kila anapofuatwa na vyombo husika kumtaafiru kwamba eneo hilo haliruhusiwi kujengwa amekuwa akikaidi na kudai kwamba yeye ni mfanyakazi wa Usalam wa Taifa. Kitendo cha kuweka Kifusi na kukisawazisha katika njia ya maji ya mto Mbezi na kimesababisha Daraja lililopo kando ya eneo hilo kuvunjika kila mara na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment