Na Lucas Raphael,Tabora
WASTANI wa watoto wa kike ni saba wenye umri
kati ya miaka tisa hadi kumi na tano hubakwa kila mwezi katika Manispaa ya
Tabora.
Msaidizi wa Dawati la jinsia la Jeshi la
Polisi Wilaya ya Tabora ,Ruth Emmanuel amesema watoto wanaobakwa wengi ni
wakatiwakitoka kwenye harusi za mitaani na kumbi za sherehe . .
Aliyesema hayo wakati akitoa mada katika
semina ya ya wajumbe kutoka kata 10 za manispaa ya tabora juu ya haki ya mtoto iliyofanyika katika ukumbi
wa mikutao wa kituo cha wanafunzi na kuandaliwa na asasi isiyokuwa ya
kiserikali ya goodness orgazation
Ameeleza kuwa wastani huo ni ule tu
unaotolewa taarifa polisi huku asilimia kubwa ya wanaotoa taarifa polisi,
wakifungua kesi ili wapate matibabu na mara baada ya kupata matibabu huwa
hawarudi kuendelea na kesi, wakiwa wametoa anuani za uongo.
Ruth Emmanuel amebainisha kwamba watu wenye
kumbi za starehe ni miongoni mwa wanaochangia ubakwaji wa watoto kwa kuruhusu
waingie kwenye kumbi kinyume cha sheria inayokataza watoto chini ya umri wa
miaka kumi na nane kuingia kwenye kumbi za sharehe na kwamba elimu inabidi
izidi kutolewa kwao ili wafuate sheria.
Kwa upande wake bibi maendeleo ya jamii,
Manispaa ya Tabora Zena Kapama ametupa lawama kwa wazazi kuwa hawatoi umuhimu
wa malezi kwa watoto wao na ndio maana huwaachia watembee ovyo hadi usiku wa
manane na kupata matatizo.
Alisema kwamba malezi ni kusimamia madili ya
watoto kwani bila kufanya hivyo hakika watoto watakuwa na malezi mbaya sana ,hakuna jinsi ya
kuthibiti vitendo na mienendo mbalilmbali ya watoto mara wafikapo nyumbani .
Amewataka wazazi na walezi kutoa umuhimu kwa
watoto wao ili wapate malezi bora na hivyo kuepukana na matatizo yakiwemo ya
kubakwa.
Hata hivyo bibi maendeleo huyo alisema kwamba
sio kila kitu unamtaka kuamuachia mtoto bali kunavitu vingine sio vya kumuachia
mtoto pekee yake .
Mwisho
.
No comments:
Post a Comment