Sunday, December 16, 2012

MADEREVA WA MAGARI NA PIKIPIKI WAPATIWA MAFUNZO



NA LUCAS RAPHAEL,TABORA

JUM LA ya madereva wa magari wapatao 779 na madereva wa Pikipiki 73 mkoani Tabora wamepatiwa mafunzo ya udereva katika kipindi cha miezi saba iliyopita mwaka huu.

Hayo yameelezwa mjini Tabora na mkurugenzi wa Mamlaka ya mafunzo ya ufundi stadi VETA kanda ya magharibi Hildegardis  Bitegera , kwenye ufunguzi wa mafunzo kati ya VETA na waajili kutoka mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Mkoa mpya wa Simiyu.

Bitegera amesema kwamba mafunzo wameweza kufanikisha kutokana na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya VETA na Jeshi la Polisi katika mikoa husika.

Aidha ametoa wito kwa wananchi wa mkoa ya Tabora na kigoma kuvitumia vyuo hivyo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kumiliki fursa za maendeleo yao binafsi nay a taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi huyo wa VETA amewakumbusha madereva wa vyombo vya moto, kuwa suala la kupata mafunzo ya ugereva kila mara ni muhimu kwa kuwa kufanya hivyo itasaidia kwa kiasi furani kupunguza ajali za barabarani.

Amesema kuwa iwapo magereva hao watazingatia kanuni na sheria za usalama barabarani kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kupunguza ajali, pia na kuokoa pato la taifa linalotumika katika kutibu majeruhi, mafao ya kifo pamoja na bima zinazoambatana na matukio kama hayo.

                                     

No comments:

Post a Comment