Mwenyekiti
wa Wama mama Salma Kikwete akikata utepe kama ishara ya kukabidhi
vitanda 80 kwa uongozi wa Hospitali ya Muhimbili leo, kulia ni Waziri wa
Afya na Ustawi wa jamii Dk. Hussein Mwinyi na kushoto ni Mkurugenzi wa
Hospitali ya Muhimbili Dk Marina Njelekela.
Mama
Salma Kikwete akisoma hotuba yake mara baada ya kukabidhi vitanda 80
katika hospitali ya Muhimbili leo (kushoto) ni Waziri wa Afya na Ustawi
wa jamii Dk. Hussein Mwinyi na kulia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya
Muhimbili Dk Marina Njelekela.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk. Hussein Mwinyi akisoma hotuba yake.
Mkurugenzi
wa Hospitali ya Muhimbili Dk Marina Njelekela akimshukuru mama Salma
Kikwete mara baada ya kupokea msaada wa vitanda hivyo leo.
Baadhi ya Mganga na wauguzi wa hospitali ya Muhimbili wakishuhudia tukio hilo.
Mama
Salma Kikwete akiongozwa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili Dk.
Marina Njelekela kushoto wakati akielekea wodini kuwatembelea wagonjwa,
kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na
katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi.
Mama
Salma Kikwete akimjulia hali Anna Razalo kutoka Nyegezi Mwanza mmoja wa
wagonjwa wa moyo aliyelazwa hospitalini hapo.PICHA NA
FULLSHANGWEBLOG.COM
No comments:
Post a Comment