Wednesday, December 5, 2012

CCM SINGIDA YAOMBA USHIRIKIANO KWA MATHEHEBU YA DINI

 Baadhi ya viongozi wa dini wakiwa mkutano baina yao na uongozi wa CCM Mkoa Singida
 Katibu CCM Mkoa Naomi Kapambala akiomba ushirikiano kati ya CCM na viongozi wa madhehebu ya dini
 Mmoja wa viongozi wa dini, Omari Hamza akitoa mchango wake wa mawazo katika kukijenga Chama kwa ajili ya maendeleo ya mkoa 
Mwenyekiti CCM Mkoa Singida, Mgana Msindai akizungumza na viongozi wa dini
Shekhe Wilaya Singida, Issah Simba akieleza matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya Singida mktk mkutano baina ya viongozi 

Na: Elisante John Singida.
VIONGOZI wa madhehebu ya dini wameombwa kuhubiri waumini wao upendo na amani, ili kuiepusha nchi kuingia kwenye.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa Singida Mgana Msindai, ametoa wito huo kwenye kutano baina yake na viongozi hao uliofanyika jengo la CCM Mkoa.

Alisema, baadhi ya wanasiasa wanaonekana kutokuwa nia njema na nchi hii, kutokana na kauli zao majukwaani dhidi ya uchochezi dhahiri wanaofanya mbele ya jamii wanayoiongoza.
Alisema kutokana na siasa chafu zinazofanywa na baadhi ya vyama vya siasa, inaweza kusababisha vurugu na hivyo kuwepo kwa uvunjifu wa amani.

Mkutano huo ni mwendelezo wa kupokea kero na ushauri mbalimbali kutoka kwa jamii ya wakazi wa Singida mjini, kabla ya kuendelea na mikutano kama huo, kwenye wilaya zingine za mkoa huo.



Kutokana na hali hiyo, mwenyekiti huyo aliwatumia fursa hiyo kuomba ushirikiano baina ya CCM na madhehebu ya dini katika kukabiliana na tatizo hilo, pia kushirikiana na serikali ya CCM kuwaondolea wananchi kero zinazowakabili.



Hata hivyo baadhi ya viongozi wa dini akiwemo shekhe wa Singida mjini Issah Simba, Musa Mpahi,Jackson Mwankolo na Daudi Mpinga walimwomba Msindai atumie mamlaka aliyonayo katika kuwaondolea wananchi kero zinazowakabili.


Baadhi ya kero hizo ni serikali kuangalioa uwezekano wa wananchi kuingizwa katika mfumo wa bima ya afya kwa ajili kunufaika na huduma za tiba, kuboresha sekta ya elimu na afya, pia kupeleka huduma ya maji safi na umeme katika kijiji cha Mwankoko.



Akijibu hoja hizo, mwenyekiti huyo alisema kuwa atajitahidi kuzifikisha katika mamlaka husika, kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi, huku akiwataka waendelee kuwa wavumilivu wakati kero hizo zikishughulikiwa.

No comments:

Post a Comment