Na Lucas Raphael,Tabora
KIWANGO cha mvua katika Mkoa wa TABORA kimeshuka
kutoka wastani wa Milimita 1500 kwa Mwaka hadi kufikia Milimita 600 Mwaka huu,
hali inayosababisha maeneo mengi ya Mkoa huo kupata ukame na kutishia kushuka
kwa uzalishaji wa Mazao ya Chakula.
Kiwango hicho cha mvua kimeshuka kutokana na
mabadiliko ya hali ya hewa, lakini kwa Mkoa wa TABORA kiwango cha mvua
kinaendelea kupungua Mwaka hadi Mwaka kutokana na uharibifu mkubwa wa Mistu
unaofanywa na uvamizi wa shughuli za kibinadamu.
Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Fatma Mwassa amewahamasisha Wananchi wa maeneo yote yenye ukame kuanza kupanda
mazao yanayostahimili ukame kama Mhogo, Mtama, Viazi vitamu na Alizeti na Ofisi
yake itatoa mbegu bure za Alizeti na Mhogo kwa maeneo yenye mahitaji makubwa.
Alisema kwamba licha wa kutoa mbegu hizo kwa
wilaya ambazo zinahitajinmakubwa laikini aliwataka wananchi kukitumia chakula
kilichonacho kwa sasa kwa ugalifu mkubwa
.
Alisema kwamba tayari hali siyo nzuri kulinangana
na mvua ilivyo kwa sasa kwani bila kuchukuliwa kwa hatua za tahadhari hali
itakuwa ni mbaya zaidi kwa jamii .
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa amewataka wakuu wa
wilaya kuwahimiza wananchi kulima mazao ambayo yastahili ukame ilikukabiliana na tatizo ambalo linaweza
kujitokeza baaday iwapo mvua itaendelea kuwa kama
ilivyo sasa.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa TABORA
ametoa Mizinga ya kisasa 130 ya kufugua nyuki yenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni Tatu na laki tisa (Mil. 3.9) ili kuwawezesha Vijana kuendesha
shughuli za ufugaji nyuki na kujikwamua kiuchumi na Kikundi cha Wafugaji nyuki
cha IPOLE kimepewa mizinga 30 ili kukiwezesha kufuga kisasa.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya Ya Sikonge Hanifa
Selengu na Katibu wa Kikundi cha Wafuga Nyuki Ipole Jabiri Nassoro wamesema
Mizinga hiyo itawawawezesha kufuga kisasa na kupata Asali nyingi itakayowandoa
katika umasikini.
Mwisho
No comments:
Post a Comment