NA Lucas Raphael,Sikonge
MKUU wa Wilaya ya Sikonge
mkoani Tabora ,Hanifa Selengu amewataka wanafunzi wa shule za sekondari
wilayani humo,kusoma kwa bidii, ili waweze kujiongezea nafasi kufauru vizuri
masomo yao.
Amesema kama wanafunzi hao
watatumia muda wao mwingi kujisomea watajiongezea nafasi kubwa ya ufauru katika
masomo yao na
hivyo kuhimili vilivyo maisha ya dunia ya sasa ya Sayansi na teknolojia.
Mkuu huyo wa wilaya ya
sikonge amewaeleza wanafunzi hao kwamba, siri kubwa ya mafanikio katika masomo
ni kusoma kwa bidii na kutoa mfano kuwa mtu akijisomea muda mwingi
anajihakikishia kuandaa maisha ya baadaye.
Silengu ameyasema wakati
akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya Sekondari Ugunda iliyopo nje
kidogo na mji wa sikonge.
Awali mkuu wa shule ya
ugunda ,Merwa Mbiha amesema kuwa mradi huo ukikamilika ujenzi wake utagharimu
kiasi cha shilingi milioni 23,854,000.
Amesema katika ujenzi huo
Serikali kuu imechangia kiasi cha shilingi milioni 13,900,000, wakati
Halmashauri imetoa shilingi milioni 7,900,000 huku wananchi nao wakichangia
nguvu kazi ya shilingi milioni 2.4.
Hata hivyo mkuu huyo wa
shule ugunda amemweleza mkuu wa wilaya kuwa, shule yake inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa maji, ukosefu wa mabweni ya kulala wananfunzi
na ukosefu wa nishati ya umeme kwa ajili ya matumizi shuleni hapo.
Kwa upande wake mkuu wa
wilaya hiyo ,Hanifa Silengu amesema kuwa Serikali ya chama cha mapinduzi CCM
inatambua changamoto zinazozikabili shule mbalimbali hapa nchini na kuhahidi
kuzishughulikia haraka iwezekanavyo.
Amemwagiza mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo ,Paul Nkulila kuhakikisha wanatatua haraka matatizo katika
shule hiyo ili wanafunzi waeze kusoma katika mazingira mazuri.
Mwisho
No comments:
Post a Comment