Na Lucas Raphael,Tabora
WANANCHI
wa kata na kijiji cha Nsololo katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora wameiomba
Serikali kuwajengea kituo cha Polisi ili kukabiliana na matukio ya uhalifu
katika kijiji chao
Mussa
Malale na Juma Msoma ni wakazi wa kata hiyo , wamesema kwamba wameamua kutoa
kilio hicho kqwa Serikali kutokana na kuongezeka kwa ,matukio ya uhalifu
yakiwemo Ujambazi na pamoja na watu kuvuana mbao holela kutoka hifadhi ya msitu
ya Nsololo.
Walisema
kwamba kata hiyo yenye zaidi ya watu 18,248 Ambapo wanaume ni 8,215 na wanawake
wanafikia 10,038 .
Wamesema
kuwa kutokana na hali hiyo wakazi wa kijiji hicho wanaishi kwa hofu kubwa na
kuongeza kwamba serikali ione umuhimu sasa wakuwajengea kituo hicho cha ili
askari waeze kukabiliana kikamilifu na wahalifu hao.
Aidha
wameeleza yakwamba kukosekana na kwa kituo hicho kimechangia kwa kiwango
kikubwa kongezeka vitendo vua uhalifu ikiwemo wizi wa kutumia nguvu.
Wananchi
hao wamesema kuwa hivi karibuni watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi walivamia
nyumbani wa mkazi mmoja waliyemtaja kwa jina moja la Mangi, alivamiwa na
kuporwa pesa ya maozo ya dukani kwake.
Katika
hatua nyingine wananchi hao wakiongozwa na Diwani wa kata hiyo Abas Kiberiti
ameiomba Serikali ruhusu kutumia mbao zinazokamatwa na maafisa misitu zitumike
kutengeneza madawati katika shule mbalimbali zenye upungufu wa vifaa hivyo.
Kiberiti
amesema kuwa inashangaza kuona mbao zionazokamatwa na maafisa misitu kuwekwa
stoo huku shule nyingi wanafunzi wake wanakosa madawati ya kukalia darasani.
Alisema
kuwa iwapo mbao hizo zitatumika kutengeza madawati tatizo la upungufu wa
madawati katika shule za msingi na kata huenda likamalizika kabisa.
No comments:
Post a Comment