Na Waaandishi wetu , hudumabongo@gmail.com
Uchunguzi
uliofanywa na wanahabari katika zoezi la kukusanya kero za sekta binafsi linaondelea
kupitia mitandao ya jamii ya Twitter na Facebook umeonyesha kuwa wakazi wa
jijini Dar es Salaam wanakabiliwa na mgao wa umeme kwa kipindi kirefu sasa.
Hali
hiyo imebainika wakati wa majumuisho ya kero za wateja wa huduma na bidhaa
mbalimbali nchini Tanzania katika
mzunguko wa tatu ambapo Shirika la Ugavi wa Umeme TANESCO limechukua nafasi ya
kwanza kati ya biashara 36 zilizotajwa kuwa kero kwa wateja.
Jumla
ya kero tofauti 220 zimewasilishwa na wateja toka zoezi hilo lianze ambapo
Shirika la Tanesco lina jumla ya kero 71 ambapo kati ya hizo 60 ni kutoka Dar
es Salaam pekee. Katika
mzunguko huu nafasi ya pili ilishikiliwa
na Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo yenye kero 63 kati ya 220 huku nafasi ya tatu ikiwaendea Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom yenye kura
17 kati ya 220 zilizowasilishwa.
Hakukuwa
na mabadiliko makubwa katika makundi mengine ambapo washindi wa kero ni
wafuatao Precision Air ( Huduma za Anga) CRDB (
Huduma za Kibenki) StarTimes
(Ving’amuzi) DAWASCO ( Huduma za Maji Safi na Taka mkoani DSM) SHOPRITE- ( Wauzaji wa bidhaa mbalimbali)
Katika
mzunguko huu jumla ya biashara 4 zimeingia katika mchuano huo nazo ni Mara
Milk, Zanzibar Insurance, Bonjour Petrol
Station na Coca Cola (Nyanza Bottlers)
Kwa
maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kura na zoezi hili linavyofanyika tembelea
link ifuatayo http://bit.ly/10SARH1
Huduma
Bongo inatoa wito kwa vyombo vya habari nchini kufuatilia kwa makini kero hii ya
mgao wa umeme unaofanyika kwa siri na utaalamu wa hali ya juu na kuleta usumbufu
mkubwa kwa wanajamii na hasara kwa wafanyabiashara.
No comments:
Post a Comment