Wednesday, December 12, 2012

DC AWA WEKA NDANI WATUMISHI MASAA 24.



NA LUCAS RAPHAEL,NZEGA
  
KATIKA Hali isiyo ya kawaida Mkuu wa wilaya ya Nzega,Bituni Msangi juzi aliwaweka ndani watumishi wa nne wa halmashauri ya wilaya ya Nzega kwa kukaidi kusimamia usafi katika maeneo yao waliyo kuwa wamepangiwa katika vikao kadhaa vilivyo pita.
 
Akizungumza kwa njia ya simu yake ya mkononi mkuu huyo alisema kuwa alifikia hatua hiyo ya kuwaweka ndani watumishi hao kwa masaa 24 kutokana na kukaidi maagizo yake yakuhusu usafi kwa nyakati mbalimbali.
 
Alisema kitendo hicho hakukifurahia kuwaweka ndani kutokana na kuwa ni watu wazima lakini kwa kukaidi maagizo hayo mpaka kupelekea mazingira ya mji huo kuwa mchafu ilimbidi awaweke ndani ili iwe fundisho kwa wengine watakao kaidi maagizo mengine.
 
‘’Ndugu mwandishi sikupenda kufanya hivyo lakini ilinibidi niwaweke ndani ili iwefundisho kwa wengine nimekuwa nikitoa maelekezo mbalimbali lakini baadhi ya watumishi hawatekelezi nimeona hiyo njia tosha na hili nitalifuatilia zaidi na kulifikisha katika uongozi wa ujuu’’alisema Mkuu huyo wa wilaya nzega.
 
Aliwataja waliowekwa ndani kuwa ni Charles Mtuka,Hamis Kyenche, Sostenes Sweya hao wakiwa watumishi wa Idara ya Afya pamoja na Emmanuel Mzile mhasibu mipango.
 
Mkuu huyo alisema kuwa zoezi hilo bado lina endelea kwa baadhi ya watendaji hata hivyo mkuu huyo hakuwataja watu hao ambao wata shiriki katika zoezi hilo la kukaa ndani kwa muda huo wa masaa 24.
 
Akizungumzia hali ya usafi katika mji huo alisema kuwa jitihada za kuhakikisha mji unakuwa safi zimeanza kwa kasi huku magari kadhaa yaki  safisha mji.
 
Bituni aliwataka watumishi wote wilayani hapa kufanya kazi na kutoa report kama walivyo panga katika vikao vyao pamoja na kuongeza juhudi katika idara zao pamoja na kutii maagizo yatayo kuwa yakitokea.
 
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri Chattar Lulenge aliupoulizwa juu ya tukio hilo alisema kuwa hayo yalikuwa maagizo ya mkuu wa wilaya hata hivyo hakuwa amekabidhiwa ofisi hiyo.
 
Akizungumzia chanzo cha tatizo hilo la usafi alisema kuwa Halmashauri imejipanga kukabiliana na tatizo hilo huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wakutosha katika kuhakikisha maeneo yote yanakuwa safi.
 
Hata hivyo jitihada zakuwapata watumishi hao waliowekwa ndani kuzungumza baadhi yao walikuwa wakiendelea na kazi hawakuweza kuzungumzia suala hilo huku wengine wakitoa ahadi ya kuzungumzia suala hilo.
 
Taarifa kutoka polis zilithibitisha kupokea watu hao wanne na kuwawekwa ndani kwa masaa 24 hukuwakidai kuwa hilo lili kuwa nia agizo la mkuu wa wilaya kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.
 
Mwisho.

No comments:

Post a Comment