Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopha Chiza(katikati),
akisisitiza jambo katika kikao hicho cha uongozi wa KNCU. Pia waziri
aliomba KNCU ikubali kuendelea kupokea wanaushirika toka maeneo mengine
nchini,na nje ya nchi, wanaopenda kujifunza zaidi kuhusu mbinu KNCU
inazotumia, inachokifanya kuwa chama kikuu kikongwe Afrika, chenye
takribani miaka 80 tangu kuuanzishwa kwake. Kulia ni Mwenyekiti wa
Bodi Bw.Maynard Swai, na kushoto ni mkuu wa wilaya ya Moshi, Dkt.Ibrahim
Msengi.
Bw.Maynard Swai (kulia)akimkabidhi zawadi, kwa niaba ya KNCU moja ya wasaidizi wa Mh.Waziri.
Bw.Maynard Swai, akiwasilisha
hotuba kwa Mh.Waziri, juu ya shuhuli za KNCU ikiwamo mradi wa Afya
unaoendeshwa na chama hiki, ambao ni mahususi kwa wakulima ambao ni
wanachama wa KNCU.
Wafanyakazi
wa KNCU (1984)Ltd, pamoja na wajumbe wa bodi ya KNCU Bw.Martin Malya
(mwenyemiwani) na Bw.Silayo(wa pili kulia),wakifuatilia jambo katika
mkutano huo.
Wafanyakazi wa KNCU (1984) Ltd, wakila chakula cha pamoja na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Coffee Tree Hotel.
Waziri wa
Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopha Chiza(kulia) akikaribishwa
na Mwkt wa KNCU Maynard Swai (kushoto), pamoja na mkuu wa Wilaya ya
Moshi(katikati) Dkt.Ibrahim Msengi, katika hoteli ya KNCU ya Coffee Tree
Hotel, mjini Moshi, tarehe 30 Nov. 2012
No comments:
Post a Comment