Na Lucas Raphael,Tabora
Wananchi mkoani Tabora wamezilalamikia mahakama
mkoani hapa kwa kuchelewesha kutoa hukumu katika mashauri mbalimbali yanayo
wakabili watuhumiwa walijazana katika mahabusu mkoani Tabora.
Hayo yalisemwa na wajumbe wa kamati ya maadili na
nidhamu ya mahakama ngazi ya mkoa katika kikao cha maadili kilichoketi
mwishoni mwa wiki kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa mtemi Isike
Kamanda wa Takukuru mkoa wa Tabora,Leonard Mtalai ambaye
ni
mjumbe wa kamati hiyo alisema kuwa
baadhi ya mahakama zimekuwa zikichelewesha kesi za watuhumiwa na kusababisha
msongamano mkubwa wa mahabusu katika magereza.
Alisema kuwa muda muafaka umefika kwa vyombo hivyo
kutoa haki za wananchi mapema ikiwa na upelelezi kwa jeshi la polisi kufanyika
mapema ili hukumu kwa haraka zifanyike
tofauti na sasa.
Kikao hicho kikihudhuriwa na wadau mbalimbali
mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Tabora Fatuma Mwassa
alisema kuwa vyombo hivyo vya mahakama vitoe hukumu mapema kwa kuzingatia
utendaji haki kwa kila mtuhumiwa.
Alisema mahakama hizo zinasheria zake ambazo
zinafuatwa na kuheshimika hivyo kanuni hizo na sheria zifuatwe ili wananchi
wapate haki zao kwa muda muafaka.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa mpango maalumu
wakuzungumza na Halmashauri za wilaya zichangie katika kukarabati majengo ya
mahakama ikiwa na makazi ya watumishi wa mahakama hizo unatarajiwa kuanza.
Hata hivyo katika kikao hicho hakimu mkazi
hakuweza kupatikana ili kutoa ufafanuzi zaidi wa kuchelewesha mashauri ya
watuhumiwa yanayosababisha msongamano wa watuhumiwa magerezani ambao wapo
mahabusu.
Hata hivyo Ofisa magereza wa mkoa hakuweza kufika
katika kikao hicho ilikutoa ufafanuzi zaidi juu ya msongamano wa magereza
mkoani hapa ambapo gereza la nzega linadaiwa kuwa na msongamano mkubwa wa
watuhumiwa kuliko uwezo wake.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment