Na Lucas Raphael,Tabora
SERIKALI Mkoani
TABORA imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya kurukia Ndege kwa
kiwango cha lami katika Uwanja wa Ndege wa TABORA ambao awamu ya kwanza
itagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 11.6.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Fatma Mwassa ametembelea eneo la Mradi na kuelezea kuridhishwa kwake na kasi ya
ujenzi wa Barabara ya uwanja huo yenye urefu wa mita 1900 ambayo kukamilika
kwake itakuwa chachu ya kukua kwa uchumi wa Mkoa wa Tabora.
Mwassaa ameseama kwa
muda mrefu wananchi wa Mkoa wa Tabora wamekosa usafiri wa anga kutokana na
kufanyika kwa ujenzi wa uwanja huo ambao ulianza kufanyiwa matengenezo Desemba
15, mwaka jana na Kampuni ya ujenzi ya Sino hydro ya kutoka China.
Alisema ujenzi wa
uwanja huo ukikamilika, ofisi yake itashiriki kuwahamasisha makampuni ya
usafirishaji wa anga kupeleka ndege zao katika mkoa wa Tabora ambao una watu
wengi wanaotumia usafiri huo wakiwemo Watalii wa uindaji wanatembelea mapori ya
hifadhi ya wanyama pori
mkoani humo.
Mhandisi Mshauri wa
Mradi huu Isack Shayo alimweleza Mkuu wa mkoa kuwa mradi huo umegawanywa kwa
awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza ni ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu
wa Mita 1900.
Alisema awamu hii
inatarajiwa kukamilika Mwezi Machi Mwaka 2013, lakini Ndege zinaweza kuanza
kuutumia Uwanja huo Mwezi Januari mwakani.
Naye Meneja wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mkoa wa Tabora Ezekia Mwalutende amesema ujenzi wa
Uwanja unaonyesha matumaini makubwa, hivyo anatoa wito kwa Wasafirishaji wa
Anga kuanza kufikiria kupeleka huduma hiyo Mkoani TABORA.
Baadhin ya Wananchi mbalimbali
wa mkoa wa tabora waliozungunza na gazeti hili wamesema kukamilika kwa uwanja
huo wa ndege kutasidia kukua kwa uchumu wa mkoa huu na hata kupata usafiri wa
haraka hasa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo.
Walisema kwamba
usafiri huo utapunguza machungu ya
ujenzi wa barabara unaondelea taratibu na sasa usafiri wa ndege kuwa jibu la
matatizo ya usafiri katika mkoa huu ,ambapo kipindi cha masika tabbora inakuwa
kisiwani.
Mwisho
No comments:
Post a Comment