Hapa mdau Mkuu wa Thehabari.com (kulia) akipata picha ya kumbukumbu na watoto katika eneo la Kibaoni Korogwe Vijijini juzi
Hata hivyo si watoto wa familia zote wamekubwa na ugonjwa huo, wapo
ambao wanaangaliwa kwa karibu na familia zao kama wanavyoonekana baadhi
ya watoto katika picha hii.
Baadhi ya watoto wanaoshambuliwa na ugonjwa wa funza. Kuanzia mtoto
wa pili kutoka kulia ni miongoni mwa familia zinazoshambuliwa na ugonjwa
wa funza eneo la Kibaoni Korogwe Vijijini.
---
Na Mwandishi wa Thehabari Korogwe Vijijini
BAADHI ya watoto wanaokosa uangalizi wa karibu
kutoka kwa wazazi au walezi wao wamekubwa na ugonjwa wa kushambuliwa na
funza kwa kiasi kikubwa miguuni na mikononi hali iliyosababisha
kuharibika kwa miguu yao na mikono kiasi kikubwa.
Idadi kubwa ya watoto walioathiriwa na wadudu hao wameonekana katika
eneo la Kibaoni Korogwe vijijini, ambapo baadhi walipohojiwa na
Thehabari walizitupia lawama familia zao kwa kutowaangalia kwa karibu
kiasi cha kushambuliwa na funza. Kassim (si jina lake sahihi) anasema
nyumbani kwao watoto wote wameshambuliwa na funza kuanzia miguuni hadi
mikononi hali ambayo imewanyima kuwa huru katika kujumuika na wenzao.
“Wadudu hawa wanawasha na kuleta maumivu makali kiasi ambacho
hushindwa hata kujumuika nawenzako…huwa najaribu wapunguza na kumsaidia
mdogo wangu pia lakini wanatuzidi ni wengi,” anasema mtoto huyo. Hata
hivyo mbali na maumivu na kuwashwa mfululizo, mikono ya kijana huyu
imeshambuliwa vibaya na funza kiasi kinachomnyima uhuru wa kuitumia
mikono vizuri kushikia vitu anuai kutokana na maumivu.
Ardhi ya kibaoni ni ya udogo mwekundu wenye vumbi hasa kipindi cha
kiangazi. Baadhi ya watu wanasema wadudu aina ya funza wanaoshambulia
binadamu ustawi zaidi katika mazingira machafu na yenye vumbi kiasi
kikubwa. Watoto na hata watu wanaoshambuliwa na wadudu hao wanaishi
katika mazingira kama hayo. Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment