Na
Lucas Raphael,Tabora
WAKULIMA
wa zao la tumbaku kutoka chama cha msingi Ipole wilaya ya Sikonge mkoani
Tabora, wametoa kilio chao kwa Serikali kufuatia kucheleweshewa malipo yao baada ya kuuza
tumbaku, miezi minne iliyopita.
Wakitoa
kilio chao mbele ya mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatuma Mwassa wamesema kuwa tangu
wauze tumabku hiyo mwezi wa nane mwaka huu, hawajalipwa malipo yao hadi sasa.
Aidha
Wakulima hao wamewalaumu viongozi wa chama chao cha msingi Ipole, kwamba wao
ndiyo wamekuwa kikwazo kikubwa kulipwa fedha zao kwa wakati.
Wamesema
kuwa viongozi wa vyama vya msingi wamekuwa chanzo kikuu cha kuchelewesha malipo
ya tumbaku kwa wakulima kwa vile wamekuwa wakiwabambikia madeni ya uongo.
Wakulima
hao wa Ipole wamemweleza mkuu huyo wa mkoa wa Tabora kwamba hawaoni umuhimu wa
kuwa vyama vya msingi kwa vile vimekuwa haviwasaidii bali ni kuwanyonya, na
hivyo kufanya hali ya maisha yao kuwa nyuma kila mara.
Kufautia
hali hiyo, wakulima hao wamemuomba mkuu wa Tabora kuingilia kati sakata hilo ili waweze kupata malipo yao haraka iwezekanavyo ili waweze kujikimu.
Wamesema
kutokana na kutolipwa fedha hizo wanaishi kwa shida kutokana na kukosa fedha za
kununulia mahitaji muhimu ikiwemo chakula na madawa kwa ajili ya kutibiwa
wanapougua.
Hata
hivyo Afisa ushirika wilayani Sikonge, Ibrahim Mwarabu na Katibu wa chama cha
msingi Ipole Gabriel Kivunde wamesema kuwa kuchelewa kwa malipo hayo kunatokana
na baadhi ya wakulima kutorosha tumbaku na kwenda kuuza katika vyma vingine.
Wamesema
kwamba wakulima wengi wamekuwa wakitorosha tumbaku zao, kutokana na kuwa na
madeni rukuki waliyokopa kwenye chama husika baada ya kukopa pembejeo
mbalimbali ikiwemo mboerea na fedha tathilimu.
Wakati
huo huo mbunge wa jimbo la Sikonge, Said Nkumba amewasa wakulima wa
tumbaku mkoani Tabora kuacha kukopa hovyo ili waweze kupata malipo mengi ambapo
wakulima wengi hivi sasa, wanapata fedha kiduchu na wengine kukosa
kabisa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment