Mkurugenzi
wa Fullshangweblog.com Bw. John Bukuku kushoto akipokea tuzo hiyo
kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki katika
maonyesho ya World Travel Market (WTM)Nchini Uingereza mwezi Oktoba
mwaka huu katikati ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utaii Tanzania TTB Bw.
Geofrey Meena.
.........................................................
Mwaka huu Fullshangwe imefanikiwa
kupata Tuzo ya kutangaza utalii wa ndani wa Tanzania kimataifa mwaka
2011 nchini Uingereza inayoitwa TANZANIA TOURISM BOARD WEB TRAVEL
MAGAZINE AWARD 2011, Fullshangweblog.com kupitia kwa mkurugenzi wake
Bw. John Bukuku ilipokea tuzo hiyo katika maonesho ya utalii ya
kimataifa ya dunia World Travel Market (WTM) yaliyofanyikaneo katika
eneo la Exel jijini London nchini Uingereza kuanzaia Oktoba 5 mpaka 8
2012, ambapo Fullshangweblog.com ilikuwa moja ya makampuni yaliyoshiriki
katika maonyesho hayo katika kupasha habari.
FULLSHANGWEBLOG.COM inaushukuru
uongozi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inayoongozwa na Mkurugenzi
Mwendeshaji Dk Aloyce Nzuki, Mkurugenzi wa Masoko Devotha Mdachi ,
Meneja Masoko Bw. Geofrey Meena na wafanyakazi wote wa bodi hiyo,
pamoja na wadau wake wote kwa kutambua mchango wa FULLSHANGWE.BLOG kama
web magazine iliofanya kazi nzuri ya kutangaza utalii wa ndani mwaka
2011 na kuitukukia tuzo hiyo, ninawashukuru sana kwani maana ya tuzo hii
ni kwamba tunamaliza mwaka 2012 kwa mafanikio.
Kuna baadhi yamambo niliyokumbana
nayo katika kazi zangu za kila siku ” Kuna matukio mengi niliwahi
kukutana nayo katika shughuli zangu za kutafuta habari mengine yalikuwa
ni ya kukatisha tamaa sana, lakini sikukata tamaa niliendelea kukaza
buti kadiri mungu alivyonijalia, Lakini mengine yalikuwa ni ya
mafanikio yenye kutia moyo.
Katika kazi hii nimekumbana na
mambo mengi “Kuna wakati marafiki zangu wa karibu walinikatisha tamaa na
kuniuliza kwamba ninafanya nini mbona sieleweki hasa wakati
nilipojitambulisha katika mikutano mbalimbali kwamba nawakilisha
WWW.FULLSHANGWEBLOG.COM wengi hawakunielewa hata kidogo nini
ninachokifanya, hata hivyo niliendelea na juhudi zangu mpaka walipoanza
kutambua na kuelewa kwamba nilikuwa nafanya nini”
Siku moja nilisafiri kuelekea
nyanda za juu kusini mkoani Iringa nilifika katika wilaya Mufindi
Mafinga nilikutana na kisa ambacho pia nilikiripoti kwenye mtandao, kisa
hiki kilikuwa hivi.
MAPANDA HOTEL WANASEMA LAPTOP COMPUTER INAKULA UMEME KULIKO PASI NA FRIJI!
Nimeingia katika hoteli hii
ya Mapanda Hotel and Guest House mjini Mafinga ili niweze kupata
kifungua kinywa lakini pia niweze kufanya kazi zangu kwenye kompyuta
yangu ya mkononi, lakini sikupata kifungua kinywa wala kufanya kazi
yoyote, Kilichonipoza ni kutumia Kompyuta yangu (Laptop) Meneja wa
Hoteli hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alinifuata na kuniambia
kwamba siwezi kuendelea kutumia kompyuta yangu kwa kuwa inakula sana
umeme ni sawa tu na friji au pasi ya umeme, hivyo ningeweza kumaliza
umeme wao wa LUKU, nikajaribu kubembeleza lakini meneja huyo
alinikatalia kabisa..
Binafsi sikujali sana wala
sikukubaliana na hoja yake manake nilijua kwamba umande na umbumbumbu
umewajaa kwenye ubongo wao katika teknolojia ya Kompyuta hivyo kwao wao
Kompyuta ya mkononi au Laptop ni sawa usiku wa giza, Ikabidi niondoke
hapo lakini bahati nzuri nikapata Internet Cafe inayoitwa 3A Traders
Internet Cafe hapo nikafanya kazi yangu vizuri kabisa
Nawatahadharisha ndugu zangu
mnataka kuja na kompyuta zenu hapa Mafinga msijisumbue kwenda hapo
Mapanda Hotel kwani yanaweza kuwapata yalionipata mimi.
MATUKIO YA KUKUMBUKWA
Kati ya matukio ambayo ni ya kumbukumbu kubwa ni tukio la kuzama kwa
September 10, 2011 ambalo mtandao wa Fullshangweblog.com uliripoti kwa
ufupi na kuvuta hisia za watembeleaji wengi MELI ya Spice Islander
imezama usiku wa kuamkia leo ikiwa safarini kuelekea Pemba ikitokea
bandari ya Malindi Unguja.
Meli hiyo inasemekana ilikuwa na abiria wapatao 610 ambapo juhudi za kuokoa majeruhi wa ajali hiyo bado zinaendelea hivi sasa.
Akizungumzia ajali hiyo,
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi amesema tukio
hilo limetokea saa 8:30 za usiku.
Haji Ussi amesema meli hiyo
iliondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima,
lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubinuka na
hatimaye kuzama kabisa.
Lakini pia tukio linguine
lililovuta hisia za watembeleaji wengi lilikuwa ni kifo cha Mwigizaji
Maarufu nchini Marehemu Steven Kanumba watu wengi walikuwa wakitembelea
mtandao ili kupata taarifa mbalimbali juu ya msiba huo.
NINAJISIKIA VIZURI KUWA BLOGGER
Nimekuwa nikifurahia kazi yangu na kuipenda sana kwani katika
kazi yangu hii ya kupasha habari imenikutanisha na watu wengi maarufu,
wasio maarufu lakini ni muhimu katika jamii na wakati mwingine
ninaposafiri katika mikoa mbalimbali na vijiji na nje ya nchi, kitu
kikubwa kinachonifurahisha ni matukio halisi ninayokutana nayo, kwani
nakutana na habari mabazo zinagusa hisia za wasomaji na watembeleaji wa
mtandao na pia zinanifanya kujifunza mambo mengi yanayotokea duniani
pia napata habari zaenye uhalisia wa maisha ya mtanzania na matukio
yenye kuvuta hisia kwa wasomaji wetu, jambo ambalo linanifanya nijisikie
vyema zaidi ninapopata nafasi ya kupiga picha na kuandika habari za
kijamii kutoka vijijini katika mikoa mbalimbali na mataifa mbalimbali
hii ni kutokana na mvuto wa picha na habari zenyewe lakini pia ninapata
changamoto za kimawazo na jinsi ya kujikwamua katika maisha ya kila
siku.
SHUKURANI KWA WADAU
Mwisho ninawashukuru wadau wote waliofanikisha hapa kwa njia yoyote ile
mafanikio ya mtandao wa FULLSHANGWEBLOG.COMsi kwa juhudi zangu binafsi
juhudi binafsi, bali pia ni juhudi za wadau wote ambao tulishirikiana
nao na tunaendelea kushirikiana nao kwa moyo wa dhati, ni matumaini
yangu kwamba tutaendelea kushirikiana kwa karibu ili tuweze kuendeleza
juhudi za kujenga nchini yetu nzuri ya Tanzania na kupasha habari zaidi
kadiri tutakavyojaliwa na Mwenyezi Mungu katika mwaka ujao wa 2013
Lakini naomba nitaje baadhi ya
taaisisi, mashirika na wadau kadhaa waliotusaidia na wanaendelea
kutusaidia kwa kututumia habari na matukio mbalimbali, ninatoa shukurani
kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Idara ya Habari Maelezo,
Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Kitengo cha habari Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kitengo cha Habari Ofisi ya Makamu wa Rais, Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB),Kitengo cha habari Ofisi ya Bunge, Vitengo vya habari
Katika Wizara mbalimbali, Mashirika, Makampuni binafsi, Idara za
serikali na wadau mmoja mmoja waliotusaidia kupata habari mbalimbali
muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.
Nitakuwa siyo mwingi wa fadhila
kama sitawashukuru kaka zangu Muhidin Issa Michuzi na Maggid Mjengwa,
kaka zangu walionitangulia kwa umri na kazi ya kublogu ninawashukuru kwa
ushauri wo ninaoweza kuuita maalumu pia kwa msaada wao katika
kunielekeza mambo mengi juu ya uelewa wa kublogu, ambao nimekuwa
nikipewa wakati wote, nashukuru sana kaka zangu naomba tuendelee na moyo
huohuo na mungu atatutangulia katika yote, Lakini pia niwashukuru
mablogger wenzagu Michuzijunior wa Jiachieblog au Ahmed Michuzi kama
anavyojulikana, Mroki Mroki, Zainul Nzige, Carthbert Kajuna, Othman
Michuzi, Abdalla Mrisho, Josephat Lukaza na Mwanamke blogger mkongwe
Mamaa Shamimu Mwasha wote ninawapenda sana
Mwisho napenda kumshukuru dada
yangu, mwandishi wetu na mpiganaji Gladness Mushi wa FULLSHANGWEBLOG.COM
mkoani Arusha, ninakushukuru dada yangu kwa kuipigania FULLSHANGWEBLOG
na kuitambulisha kwa nguvu mkoani Arusha kutokana na habari nyingi za
kijamii ambazo umekuwa ukizituma kutoka huko, tuko pamoja na FULLSHANGWE
inakuangalia kwa macho mawili Mungu akubariki sana na uwe na afya njema
ili tuendeleze kazi