Wednesday, March 20, 2013

"ASKARI POLISI WANNE WANAODAIWA KUFANYA MAUAJI YA MTU MMOJA URAMBO WAREJESHWA KAZINI KIMTINDO"


 

"INAUMA SANA SIJUI HAWA ASKARI POLISI NI WATOTO WA VIGOGO?"



HALI HALISI YA MAUAJI YA HASSAN MGALULA:

Askari Polisi hao wakati wakimchukua kwenye usafiri wa Bajaji ya mizigo huku wakiwa  wamemkanyaga bila kujali hali mahututi aliyokuwanayo marehemu Hassan Mgalula mara baada ya kipigo kikali kilichosababisha kifo chake hapo baadaye,INASEMEKANA KUWA  WALIPOFIKA  KITUONI  WALIFUNGUA  JALADA  LILILOONESHA  KUWA HASSAN  AMEPIGWA  NA  WANANCHI  WENYE  HASIRA  KALI......(Picha hii kwa hisani ya Nassor Wazambi-Aliyekuwa Mwenyekiti UVCCM wilaya ya Tabora mjini.) 

POLISI wanne waliokuwa wanaodaiwa kuhusika na tuhuma za  mauaji ya mtu mmoja huko Wilayani Urambo ambao walifukuzwa kazi baada  ya kufikishwa mahakamani imedaiwa kuwa wamerejeshwa kazini huku yakizuka maswali mengi yasiyo na majiibu  juu ya kuachiwa kwao.

Askari Polisi hao ambao walifukuzwa kazi mnamo March 5 mwaka 2012 baada ya kubainika wamehusika na tukio hilo la kinyama la kumpiga hadi kupoteza fahamu marehemu Hassan Mgalula ambaye baade alipoteza maisha ni namba  G 3037 Pc Aidano, namba G 3836 Pc Jonathan, namba G 4836 Pc Mohamed na mwingine ni namba G 5382 Pc Khakimu.

Kuachiwa na kurejeshwa kazini  kwa askari Polisi hao wanne kumezua hali ya sitofahamu kuanzia  kwa askari Polisi wenzao hadi kwa wananchi wa wilaya ya Urambo ambao waliobahatika kulishuhudia tukio la kumpiga raia huyo wa Urambo marehemu Hassan Mgalula na baadae kufariki dunia kabla ya kufikishwa kituo cha Polisi ambako lilifunguliwa jalada kwamba ameuawa na wananchi wenye hasira kali.

Aidha juhudi za kumtafuta kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Athony Rutha ili kutolea ufafanuzi juu ya kurudishwa kazini kwa askari hao zinaendelea lakini kumekuwa na dalili za utata kutokana na askari hao imeelezwa kuwa kuna mikono ya vigogo wa Jeshi la Polisi ngazi ya juu.

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Urambo kutokana na tukio la kurejeshwa kazini kwa askari hao wanaodaiwa kufanya unyama huo mnamo Februari 29 mwaka 2012 wameonesha dalili za kukosa imani na Jeshi hilo huku wakilalamikia uongozi wa Polisi ngazi za juu kwa kuendelea kuwabeba baadhi ya askari wanaotenda makosa kinyume cha sheria. 

No comments:

Post a Comment