Wednesday, March 20, 2013

RHINO RANGERS YAREJESHA LIGI KUU TABORA

NA LUCAS RAPAHEL 
 

Baada ya miaka 12 kupita hatimaye mkoa wa Tabora umefanikiwa kupata timu itakayoshirikia katika  ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara  msimu ujao wa 2013/2014 kupitia timu ya Rhino Rangers inayamilikwa na jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kabla ya  timu hiyo kuweka rekodi mpya kwa mara ya mwisho timu ya Milambo ya Tabora ilishuka ligi daraja la kwanza Tanzania bara mwaka 2000 ,timu ambayo chanzo chake ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora kwa wakati huo Dk Laurent Gama kwani alipoteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM ndio ukawa mwanzo wa timu hiyo kupoteza mwelekeo katika medani ya soka nchini.  .

Lakini historia ya soka la mkoa wa Tabora imechukua sura mpya kufuatia timu pekee ya Jeshi la wananchi Watanzania, Rhino Rangers  kujihakikishia nafasi ya kushiriki  ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kuongoza kundi C la ligi daraja la kwanza lililokuwa na ushindani wa aina yake ikiwa imefikisha pointi 29 huku ikiwa na  mchezo mmoja,pointi ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote katika kundi hilo.

Timu ambazo zilizopo  katika kundi c ni Kanembwa JKT, Polisi Dodoma, Polisi Tabora, Mwadui, Pamba, Polisi Mara, Molani ya mkoa wa Manyara na Rhino ambaye ndio mbabe wa kundi hilo.

Akizungumza na mwandishi wa makala haya mlezi wa timu hiyo ya Rhino Mnadhimu Mkuu wa Mafunzo na Utendaji wa Kivita wa Faru ya Brigedi  Kanali Simon Hongoa amesema kwamba mafanikio ya timu hiyo hayakuja  kama mvua  bali wampitia vikwanzo vingi na hatimaye mafanikio ambayo yanaonekana hii leo .

Amesema kwamba Rhino Rangers ilianza mwaka 1994 baada ya kuvunjika kwa timu ya divisheni ya 20 mwaka 1993 na kuanzia hapo Rhino ilianza kusukwa ili iwe timu ya ushindani ndani na nje ya mkoa wa Tabora.


Kanali huyo wa JWTZ  amesema kwamba  timu hiyo ilianzia daraja la nne, kupanda  hadi kufikia daraja la tatu na la  pili kupitia mfumo wa zamani wa FAT kabla ya mabadiliko  ya ushiriki wa madaraja ya soka kufanywa na shirikisho la soka nchini TFF..

Amesema kwamba katika vipindi tafauti ya mashindano hayo kunzia mwaka 1995 hadi mwaka 1999 walishindana kwa kila hali kupanda daraja la kwanza lakini walikutano na vikwanzo vingi ingawa hawakukata tamaa ya kushiriki katika ligi hiyo licha ya kuwa mabingwa wa mkoa mara kadhaa .

Katika jitiada zao waliweza kufikia nafasi ya tano kwa makundi ,kwa mfano mwaka 1998 walishiriki ligi daraja la kwanza na kufakikiwa kushika nafasi ya tano na kuachwa na timu  zingine zikipanda ligi kuu.
Katika harakati za kufanya vizuri timu hiyo ilivunjwa kwa mara nyingine  mwaka 1999 hadi mwaka 2006 ilipofufuliwa tena  baada ya ujuo wa kanali huyo wa jeshi la wananchi kufika katika kanda hii ya Magharibi.

Kanali Hongoa amesema wakati timu hiyo ilikuwa na mambo mengi yaliyopelekea  kufutwa tena kwenye anga la soka.Mwaka 2007   ilishiriki ligi daraja la tatu ngazi ya taifa na kufanikiwa kuwa bingwa wa mkoa wa Tabora mwaka wa 2008.

Amesema jitiada zao zilianza mwaka 2009 na mwaka 2010 waliweza kushika nafasi ya tano kati ya timu zilizoshiriki katika ligi ya makundi wakati huo iilifanyikia mkoa wa tanga na kufaniwa kuingiza timu za Costal Union,Villa Squad,oljoro JKT na Moro utd ..

Lakini aliendelea kusema kwamba jitihada zao  walitegemea wangeweza kupanda ligi kuu mwaka 2011 lakini walitimuliwa vumbi na timu za Polisi moro ,JKT Mgambo,na Prison ya Mbeya ambazo zilifanikiwa kuingia ligi ya kuu ya Vodacom wakati huo ligi ya makundi ilifanyika nkoa wa Morogoro..

Pamoja na vikwazo hivyo hawakukata tamaa ya kuendelea kushiriki na kuwania nafasi ya kupanda ligi kuu huku  wananchi wa mkoa wa Tabora waliweza kuwatia moyo na jitiada za wachezaji wake wamefanikiwa kuingia ligi kuu hiyo ya Vodacom  Tanzania bara.

Amesema kwa hiyo ni faraja kwa Jeshi la Wananchi kwa kupata hata timu moja inayoshiriki ligi kuu ya soka  nchini kwani timu zinazoshiriki ligi hiyo zinamilikiwa na  Jeshi la Kujenga Taifa  JKT na zinafanya vizuri kwa sasa .

Kamanda huyo kwa jina maarufu “babu” amesema kwamba jitihada zilizopo ni kuhakikisha Rhino inafanya usajiri wa kufa mtu kwani wanataka kuwa na timu bora na sio bora timu.

“hatutaki kunusa tu katika ligi hiyo na mwaka unaofuata tusiwepo hilo kwetu hatulitaki kusikia bali mshikamano kutoka kwa wananchi wa mkoa wa Tabora kwani ndio nguzo kubwa  toka mwanzo kwa ligi hii inayotarajiwa kumalizika tarehe 17 mwezi huu” .Amesema kanali Hongoa.


Ametaja kikosi kilichoweza kupandisha timu hiyo ya Jeshi la wananchi wa Tanzania kuwa makipa ni Idd Kihulya,Charles Mpinki na Abdullakarim Mtumwa.

Mabeki wa pembeni kulia na kushoto ni Salum Mambo ,James Barton ,Frank Konye ,Ally Mwanyiro ,Stanley Mlay na Joseph Mapunda.

wengine ni viungo ambao ni Stanlaus Mwakitosi ,Ramadhani Sheweji ,Emanuel Noel ,Steven Maztudd ,Bakari Maadhi na Salum Majid.

Pia amewataja viongo wa kati ni Julias Masunga, Issa Salum, Ayub Iddy, Joseph Sangadata na Ussi Makeme ,hao wakifuatiwa na washambulia wa Timu hiyo ambao ni Shija Joseph ,Magesa omary ,Doi Mobi ,Msafiri Mbilinyi, Samwel Mwamasangura,shija Mvugo Abdallh Simba,Victor Anghaya Abbas  Mohamed  na Mchembi Maganga.

Hata hivyo kanali Hongoa  amewashukuru wakazi wa mkoa wa Tabora wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora, Hassan Wakasuvi, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya ya Tabora na wadau wote wa soka ambao wamejitolea kwa hali na mali ili kufanikiwa kwa timu hiyo kufika hapo ilipofika leo.

Aidha kocha wa timu hiyo ya Rhino Renatus Shija amesema kwamba halipofika katika timu hiyo aliangali history ya  Rhino na baada ya kuangali aliweka mkakati wa kuhakikisha wana maliza raun di  ya kwanza wakiwa wanaongoza ligi daraja la kwanza na hivyo kuhakikisha watoki katika nafsi hiyo hali iliyowasaidia sana kufika hapa walipofikia.

Mara baada ya kumaliza raundi ya kwanza na kuongoza kundi C  kwa pointi 17 wakapanga kuhakikisha wanashinda michezo mitano waliyopangiwa kucheza katika uwanja wa nyumbani  wa Ally Hassan Mwinyi katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo ili waweze kuongoza na kupanda daraja jambo ambalo wamefanikiwa.

Amesema kwamba amependa ushirikiano kutoka kwa viongozi wa timu hiyo ya Jeshi na wananchi wa mkoa wa Tabora  kuwapa sapoti ya nguvu kwa wameina timu hiyo kama yako.

Kwa sasa wanampango wa kuhakikisha wanapata timu bora yenye wachezaji wenye uzoefu na ligi hiyo ,kwani ligi kuu ni mambo mengi ambayo yanabidi kuyafanyika kazi kabla ya ligi hiyo kuanza na kuongeza kwamba anataka tinu hiyo ya Rhino kuweka history ya kuchukua ubingwa wa bara mwakani .

Kapteni wa Timu ya Rhino  Shija Joseph amesema kwamba mafaniko ya timu hiyo ni mikakati ya viongozi wa jeshi hilo ,viongozi wa serikali pamoja na wananchi wa mkoa wa Tabora kwa kupatia ushirikiano mkubwa na kuhakikisha wanafika hapo walipofika leo.

Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Tabora (TAREFA)   , Yussuph Kitumbo alisema kwamba lengo la kukikisha timu mojawapo ambazo zilishirikia kwenye ligi daraja la kwanza mwaka huu mkooani hapa zinapanda  na hilo,limewezekana

 “Nina imani kuwa sisi kama TAREFA,serikali ya mkoa,wadau na wapenzi tukishikamana nina imani kubwa soka ya Tabora inakuwa kwa kasi kwani kuna vipaji vingi sana mitaani ambavyo vijana waliopo wanapaswa kuendelezwa katika michezo mbalimbali.” Alisema Kitumbo.

Amesema kwamba baada ya timu ya Rhino kufikia hapo ilipofikia basi uzalendo kwanza ili tuonyeshe mapenzi ya kweli na timu hiyo ambayo kwa sasa ni ya wana Tabora wote .

Mwisho

No comments:

Post a Comment