Wednesday, March 20, 2013

TAASISI ZA SERIKALI ZAONGOZA KWA MADENI YA ANKARA ZA MAJI TABORA

 
Na LUCAS RAPHAEL TABORA, 

MAMLAKA ya maji safi na maji taka Tabora (TUWASA), imetaja wateja wake
ambao ni wadaiwa sugu ambao ni taasisi 13 za serikali, binafsi na
taasisi za dini hadi kufikia februari 28,2013 ambao wanadaiwa zaidi ya
sh milioni 6.1.

Akisoma taarifa yake siku ya uzinduzi wa wiki ya maji katika manispaa
Tabora,mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Injinia Bwire Mkama alisema wadaiwa
sugu waliowengi ni taasisi za serikali,mashirika ya umma na taasisi
binafsi.

Injinia Mkama alitaja jeshi la wananchi wa Tanzania,(JWTZ),sh milioni
506,766,028,ikifuatiwa na jeshi la polisi sh milioni 96,612,465,ofisi
za serikali sh milioni 18,126,401,vyuo vya umm ash milioni 12,327,670
na shule za msingi milioni 11,408,598.

Aidha alitaja taasisi nyingine kuwa ni jeshi la Magereza sh milioni
9,547,815,TRC sh milioni 5,339,274,taasisi za dini ya kiislamu sh
milioni 4,427,202,hospitali ya mkoa wa Tabora,Kitete sh milioni
3,738,380,halmashauri ya manispaa Tabora 3,261,140,shule za sekondari
sh milioni 3,084,984.58,taasisi za dini ya kikristo sh milioni
1,729,195 na ofisi ya RAS mkoa wa Tabora sh milioni 1587,690.

Aidha mkurugenzi huyo alizitaja shule za msingi zinazodaiwa hadi
kufikia mwezi machi 15,2013 kuwa ni shule msingi Kiloleni sh
903,000,shule msingi jamhuri sh 539,800,shule ya msingi Gongoni sh
2,073,000.

Alizitaja  taasisi nyingine kuwa ni shule ya msingi Mkoani sh 363,000
na shule msingi Uhuru sh 1,189,550, Cheyo shule ya msingi sh 706,500
na shule ya msingi Igambilo sh 409,355.
Injini Mkama alisema inafikia mahali huduma kama za madawa wanashindwa
kununua kwa wakati kwani fedha nyingi kwa ajili ya uendeshaji inatuwia
vigumu.

Alisema hivi sasa kuna operesheni ya kudai wadaiwa sugu na
tumewasiliana na serikali ya wilaya ili watusaidie kudai madeni kwa
wateja wetu ambao na taasisi za serikali ambazo sehemu kubwa ya deni
ni taasisi hizo.

No comments:

Post a Comment