Wednesday, March 20, 2013

RADI YAJERUHI WANAFAMILIA NA KUSAMBARATISHA MAKUNDI YA MBUZI SIKONGE

 

Na Lucas Raphael  Sikonge

MVUA zinazoendelea kunyesha katika wilaya ya Sikonge, zimeleta madhara kadhaa, baada ya watu wanne wa familia moja kulazwa hospitalini kutokana na mshituko wa radi.

Akizungumza na gazeti hili diwani wa kataka Kilolelo Boniface Mlimakala Mtani, alisema tukio hilo la radi lilitokea hivi karibuni, ambapo familia hiyo ilipata mshituko na kulazwa hospitalini huku mbwa wanne na mbuzi mmoja wa familia hiyo wakipigwa radi na kufa hapohapo.

Mtani alisema kuwa tukio la radi lilitokea ,ajira ya saa nane mchana,mwezi machi 8,mwaka huu katika kitongoji cha Maweni B,kijiji cha Kanyamsenga,kata ya Kiloleli.

Aliwataja waliojeruhiwa na kulazwa hospitali,(DDH),wilayani Sikonge,kuwa ni Aloyce Masima,(45),ambaye alijeruhiwa sehemu ya mguuni kama amemwagiwa maji ya moto,Paulo James(18), Hoka Kazinza (16),na Gabriel Aloyce (2).

Mtani aliongeza kuwa familia hiyo ililazwa hospitali kwa siku moja kabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbani,kati yao watoto watatu walipata mshituko wa radi huku baba yao akibabuliwa mguuni na radi hiyo.

Akiongea zaidi diwani huyo alisema baada kupata taarifa hizo alifika nyumbani walipokuwa wakiishi na kukuta wamepoteza fahamu huku mbwa wanne na mbuzi mmoja wakiwa wameshakufa kwa kupigwa na radi hiyo.

Hata hivyo diwani huyo alisema kuwa licha ya familia hiyo moja kupigwa na radi,hakukuwa na mvua yoyote kijijini hapo zaidi ya kuwepo mawingu,huku mvua ikiwa inanyesha kilomita moja toka eneo la tukio.

Katika hatua nyingine Mtani aliongeza kuwa zoezi la kuwasaka watoto wanaotakiwa kuingia sekondari baada ya kufaulu bado linaendelea na limeanza kuzaa matunda.

No comments:

Post a Comment