Sunday, September 29, 2013

CCM TABORA MJINI WAANZA KURUMBANA,KIGOGO AFANIKIWA KUWAZUIA WANAOKISAIDIA CHAMA HICHO

Kadri joto la kisiasa linavyozidi kupamba moto mjini Tabora Kigogo mmoja wa Chama cha Mapinduzi hatimaye amefanikiwa kutumia njia ya kuwazuia wanaokisaidia chama hicho kwa kufikisha malalamiko yake kwenye kamati ya maadili ya CCM ngazi ya Taifa eti kwa madai kwamba nia yao si kukisaidia chama hicho bali ni kujiandaa kuwania nafasi ya Ubunge.

Habari za ndani tulizozipata kutoka maeneo tofautitofauti zimeeleza kuwa kigogo mmoja ambaye jina tunalihifadhi amelazimika kumtumia mjumbe mmoja wa CCM ambaye kutokana na maradhi yanayomsumbua ametumia mwanya huo wa kumshurutisha aandike barua na kuipeleka kwa mkono wake kwenye kamati hiyo ya maadili akidai kuwa wapo jamaa Tabora mjini ambao wanatumia mikutano ya hadhara kwa maandalizi ya kuwania nafasi za udiwani na ubunge mwaka 2013 kwa kuitumia jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Tabora mjini jambo ambalo ni kinyume na taratibu na kanuni za katiba ya CCM.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari hii ambavyo tunavihifadhi,Mjumbe huyo ambaye moja kati ya masharti aliyopewa kutokana na msaada wa matibabu aliopatiwa na Kigogo huyo ni kuhakikisha anaandika kwa makini malalamiko hayo ambayo hata kwenye fikra zake hakuwanayo huku akisahau kabisa  msaada wa kwanza aliopatiwa na hao alioshurutishwa kuwalalamikia  kwenye kamati ya maadili jambo ambalo pia limewachukiza wanaccm wa karibu yake ambao wamekuwa bega kwa bega katika kumsaidia adha ya magonjwa yanayomsumbua tangu awali.

Hata hivyo walalamikiwa wa sakata hilo waliofikishwa katika kamati ya maadili CCM taifa,ambao wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali kama wafanyavyo vyama vya Chadema na Cuf katika hatua ya kuviimarisha vyama vyao,wao kupitia Jumuiya ya umoja wa vijana ccm wilaya ya Tabora mjini  wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kufanyika mbinu chafu za kutaka kuwazuia kuendelea na mikutano hiyo hatua inayodaiwa kufanywa na Kigogo huyo kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi bila kujali CCM ina nafasi gani kwa wananchi wa Tabora.

Hata hivyo duru za kisiasa zinasema kuna kila dalili kwa CCM hapa mjini Tabora itaendelea kutokuwa na mvuto wa kisiasa kwa kile kinachodaiwa kuwa kuwepo kwa dhana potofu kwa baadhi ya vigogo kwamba chama hicho kinapendwa na wananchi tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere jambo ambalo wanasahau kuwa hivi sasa watu waliowengi wamekuwa na mwamko na zaidi ya yote pale vyama vya upinzani vinapotumia udhaifu wa utendaji wa Viongozi wa chama tawala ambao ndio kinaongoza serikali.

Wakati vyama vya siasa hapa mjini Tabora vikiendelea kuvuta kasi ya kujiimarisha kisiasa lakini jambo la kushangaza zaidi Chama cha Mapinduzi,Chama tawala, kimekuwa katika mivutano isiyokuwa na tija kwa Chama hicho hatua ambayo inafikia eti mmoja wa viongozi anatafuta namna ya kuzuia wenzake wasiweze hata kukutana na wananchi kusikiliza matatizo yao akihofia kuwa anaweza akapoteza nafasi yake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Baadhi ya wanaccm baada ya kutolewa amri ya kusitishwa shughuli za mikutano ya hadhara inayofanywa na Jumuiya ya UVCCM wilaya ya Tabora mjini,wameamua kutelekeza shughuli zote za chama hicho huku wakieleza kuwa liwalo na liwe hata ikibidi chama kushindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.





  

No comments:

Post a Comment