Tuesday, September 3, 2013

FAMILIA DUNI ZA WALEMAVU ZIPATIWE ELIMU NA MATIBABU BURE RASIMU YA KATIBA






MWENYKITI WA SHIRIKIKSHO LA WATU WENYE ULEMAVU TANZANIA(SHIVYAWATA) WILAYA YA URAMBO DANIEL MWITA AKIWA KATIKA MKUTANO WA KUJADILAI JUU YA RASIMU YA KATIBA MPYA KATIKA UKUMBI WA VICKITORIA URAMBO


 NA LUCAS RAPHAEL.URAMBO

Imeelezwa kwamba rasimu ya katiba mpya imamke wazi kwamba watu wenye ulemavu na watoto wao wapatiwe elimu bure kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu kwa lengo la kuweka usawa wa elimu kati ya walemavu na watu wasiokuwa walemavu sanjari na huduma za afya.
MWANASHERIA AMBAYE NDIYO ALIYONGOZA MJADALA WA WA RASIMU  YA KATIBU ABEL SENGEREMA PEMBENI YAKE NI MTOA MADA KATIKA MJADALA HUO NI JOHN PININI

Akizungumza wakatika wakichangia mjadala wa rasimu ya katiba mpya wilayani wilayani Urambo mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu wilaya ya Urambo (SHIVYAWATA) Daniel Mwita  alisema kwamba katika kipengele cha elimu kiongezwe kipengele cha elimu kwa walemavu pamoja na kupata matibabu bure .

Alisema kwamba walemavu hapa nchi waliopata elimu ni asilimia isiyozidi 5 tu na hilo linatokana na wazazi kutokuwa na muamko wa kuwapeleka watoto wao shuleni  na kupata matibabu bure kwani walemavu wengi wanakufa kutokana na kukosa matibabu na kutona na  gharama kubwa kwao.

Alisema kwamba katiba itakayokuja itamke wazi walemavu na watoto wao wapate elimu bure ili kupunguza watoto wa mitaani ambayo inatokana na wazazi wengine kutokuwa na uwezo wa kuwasomesha watoto wao .

Alsema kwamba iwapo walemavu watapata elimu na matibabu bure hata hali ya kuwaona mitaani itapungua kwani omba omba watapungua kwani itakuwa rahisi kwao kutafuta hata mikopo na kuweza kuanzisha vyama vyao vyakuweka na  kukopa saccos kwani watakuwa wamejitambua kwa kupata elimu.

Mwita alisema kwamba kutokana na hali hiyo kwa walemavu nchini kukosa elimu na matibabu yakina  kunasababiasha watu wenye wasiweza kupona kwani lemavu mwingine unaweza kutibabika iwapo mhusika hatapata matibabu kwa muda muafaka na elimu


Aidha  mwanasheria wilayani urambo Abel Sengerama alisema kwamba licha ya bunge kupata wawalikishi kutokana nafasi tano za rais kuweza kuwakilisha watu wenye ulemavu bungeni ,lakini pia  iwepo na nafasi za uwakilishi kwa watu wenye ulemavu katika mabaraza ya madiwani nchini kote  ilikuwapata watu watakao kuwa na uwezo wa kuwasema watu wenye ulemavu .

Alisema kwamba kupatikana  diwani mwenye ulemavu kutasaidia sana kupata msemaji wao katika bazara hilo ilikuweza kujua nini kinachowasumbua watu wenye ulemavu katika kata husika .

Hata hivyo walemavu hao waliomba rasimu hiyo iseme wazi juu ya kuwatengea dirisha maalumu katika hospital ,kwa lengo la kuwaraisishia kupataji,  madawa na huduma zingine .

Kikao hicho cha baraza la rasimu ya katiba yalifayika katika ukumbi wa mikutano wa Victoria wilayani humo.



No comments:

Post a Comment