Na Lucas Raphael,Tabora
ZAIDI ya vijana 40 wa kata ya shigamba
wilayani Nzega mkoani Tabora wamepatiwa mafunzo ya ujasiria mali na shirika la kazi Duniani (I L O) yatakayo
wawezesha kuwapa mwongozo wa kufanya kazi zao za ujasiria mali kwa
ufanisi zaidi.
Baadhi ya Vijana hao waliopata mafunzo hayo
walisema kuwa mafunzo hayo yamewawezesha
kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi tofauti na hapo awali walikuwa wakifanya
kazi zao kwa kutumia mazoea.
Wakitoa pongezi kwa shirika hilo la kazi Duniani (I L O) kwa kuwewezesha mafunzo hayo
ya wiki mmoja mpaka kuhitimika jana waliongeza kuwa wanauwezo mkubwa wa kufanya
biashara zao bila kupata hasara kama ilivyo
kuwa hapo awali.
Wakitoa wito kwa serikali na mashirika
yasiyo ya kiserikali Vijana hao wameiomba kuiga mfano huo na kuendeleza mafunzo
kama hayo kwa vijana ili kuwawezesha kuwa wajasiria mali wazuri ambao watafanya kazi
bila kupata changamoto ikiwa na kupunguza wimbi la vitendo viovu.
Walisema endapo mashirika mengine yataiga
mfano wa shirika hilo yatasaidia kupunguza wimbi
la ukosefu wa ajira na vijana wengi watajiingiza katika ujasiria mali iliwaweze
kujiajiri wenyewe.
Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo,
Wenceslaus Antony Msita aliwapongeza vijana hao kwa kujitolea kupata mafunzo
hayo ambayo yatawasaidia katika kuendesha miradi yao
ya ujasiria mali.
Akitoa maelezo jinsi vijana hao walivyo
patikana alisema kuwa ni vijana wenye umri wa miaka 16 hadi 45 ambao wamepata
mafunzo hayo.
Aliongeza kuwa mafunzo hayo yataendelea
kutolewa na shirika hilo kwa kata mbalimbali ili
kila kijana wa wilaya hiyo aweze kuwa mjasilia mali ikiwa na kuondokana na
umasikini.
Antony aliwataka vijana hao kuzingatia mafunzo
yote waliyopewa katika kipindi hicho cha wiki mmoja ili waweze kuwa wajasiria mali wa
kujitegemea.
Alishirika hilo
halinauwezo wa kuwakopeshe badala yake litazungumza na taasisi za kibenki ili
vijana hao waweze kukopeshwa na kuendesha miradi yao bila kupata hasara yeyote itakayo weza
kujitokeza.
Alisema kuwa vijana hao wanauwezo kubwa wa
kuendesha biashara na kuongeza kuwa taasisi hizo ziwakopeshe kwa liba nzuri
iliwaweze kurejesha mapema mikopo hiyo na kuendelea na ujasiria mali
wao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment