Thursday, January 16, 2014

DC IRAMBA AWAFUNDA MADIWANI WA MANISPAA YA TABORA KUHUSU MFUKO WA AFYA YA JAMII

 
Mkuu wa wilaya ya Iramba Bw.Yahaya Nawanda akizungumza katika mkutano wa wadau kuhusu uanzishwaji wa mfuko wa Afya ya Jamii Manispaa ya Tabora,mkuu huyo ameshiriki katika mkutano huo kwa lengo la kutoa maelezo namna Wilaya yake ilivyofanikiwa kuihamasisha Jamii kuchangia mfuko huo unaotoa huduma ya Afya kwa kutumia Kadi katika hospitali,zahanati na vituo vya afya vinavyomilikiwa na halmashauri.
Baadhi ya wadau wakiwemo Watendaji wa mitaa,Kata na vijiji wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Iramba ambapo pia aliwataka Madiwani kusaidiana na Watendaji hao kuhamasisha Jamii iweze kujiunga na Mpango huo wa Tiba kwa Kadi(TIKA)
Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya,Mwakilishi wa mkurugenzi wa NHIF Taifa Bw.Athuman Rehani na mkuu wa wilaya ya Igunga Bw.Elibariki Kingu wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Iramba katika mkutano huo wa wadau.
''Madiwani wasaidieni wananchi kujenga uchumi wao ili iwe rahisi kuwahamasisha kuchangia mfuko wa Afya ya Jamii hatua ambayo pia itawasaidia kuwajengea mazingira mazuri ya kurejea kwenye nafasi zenu kwenye uchaguzi  mkuu  wa 2015"Alisema  Bw.Nawanda.
Wadau waliendelea kuwa makini kusikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na maafisa wa NHIF/CHF.



No comments:

Post a Comment