Friday, January 17, 2014

KIKAO CHA WADAU KWA AJILI YA UANZISHWAJI WA MFUKO AFYA YA JAMII TIKA MANISPAA YA TABORA



Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa akifungua mkutano wa wadau kuhusu uanzishwaji wa mfuko wa afya ya jamii Tiba kwa Kadi Manispaa ya Tabora ambapo aliwataka wadau hao kuhamasisha jamii kujiunga na mfuko huo ambao utasaidia kupata huduma bora za matibabu pindi wanapougua.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF ambaye pia ni kaimu Mkurugenzi wa CHF nchini  Bw.Athumani Rehani akiwasilisha salamu za NHIF katika mkutano huo wa wadau ambapo alieleza kuwa mfuko huo upo tayari kushirikiana  kwa karibu katika kuchangia Maendeleo ya mkoa wa Tabora huku ukiiomba Serikali ya mkoa huo kuwapatia eneo ambalo mfuko utawekeza kwa kujenga Jengo la Ghorofa Sita.
Baadhi ya Wadau wakiwa katika ukumbi wa mkutano huo.
Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kanda ya Magharibi Bw.Emmanuel Adina akikaribisha wadau katika mkutano huo wa uanzishwaji wa mfuko wa afya ya jamii TIKA katika ukumbi wa Mtemi Isike ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Iramba Bw.Yahaya Nawanda na Mkuu wa wilaya ya Igunga Bw.Elibariki Kingu ambao walihudhuria katika mkutano wa wadau wa mfuko wa afya ya Jamii mjini Tabora.  
Wadau wakiwemo madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Tabora,Watendaji kata,mitaa na vijiji Viongozi wa dini,Wazee maarufu na Wataalamu wa sekta ya Afya wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa uanzishwaji wa mfuko wa Afya ya Jamii manispaa ya Tabora.
Diwani wa kata ya Malolo manispaa ya Tabora Bi.Zinduna Kambangwa ambaye alihudhuria mkutano huo wa wadau wa mfuko wa Afya ya Jamii.

Baadhi ya Maafisa wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao walikuwa wakihakikisha mkutano huo wa Wadau wa mfuko wa Afya ya Jamii ukiendelea vizuri katika ukumbi wa Mtemi Isike ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora.
Diwani wa kata ya Kitete Bw.Daniel Mhina alihudhuria katika mkutano huo akisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa ambazo zilionesha mafanikio makubwa ya mfuko wa Afya ya Jamii.
Maafisa wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya walipiga picha ya pamoja na viongozi wa Serikali ya mkoa wa Tabora na wilaya ya Iramba.

NA LUCAS  RAPHAEL,TABORA.

MATIBABU KWA KADI


MKUU wa mkoa wa wa Tabora FATUMA MWASSA ameiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ihakikishe upatikanaji wa huduma bora za  afya zinazotolewa  katika mpango wa matibabu kwa kadi TIKA zinazokusudiwa kutolewa kwenye manispaa hiyo.

Pia ametaka huduma za zitolewazo katika vituo vyote vya afya katika Manispaaya Tabora zinakuwa bora ikiwa ni pamoja na kuwepo Lugha nzuri kwa wanachama mfuko huo sanjali na upatikanaji wa dawa kwa wingi na vifaa tiba.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikako cha wadau wa mfuko wa afya jamii mijini TIKA, katika manispaa ya Tabora kilichafanyika katika ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi mjini Tabora.

Akizungumza katika kikao hicho, mama Mwasa amesema fedha za michango ya wanachama ni lazima zitumike kununulia dawa na kuitaka Halmashauri hiyo ihakikishe kuwa mongozo wa matumizi ya fedha hizo unafuatwa kikamilifu kwa lengo la kutimiza azima yake.

Amesema kuwa ofizi ya mkuu wa mkoa na ofisi ya katibu Tawala wa mkoa haitakubali wala hatakuwa tayari kupokea sababu yoyote ya wananchi kutopata huduma ya afya baada ya kuwa wamechangia huduma hiyo.

Mama Mwassa ameitaka Halmashauri hiyo kushirikiana na mfuko wa taifa wa bima ya afya kuendesha kampeni ya kuhamasisha wananchi ili kujiunga na mpango wa tika kwa kadi kwa lengo la kurahisisha upatikananji wa huduma za afya kwa gharama nafuu.

Mapema mkurugenzi wa CHF na kaimu mkurugenzi wa mfuko wa taifa ya bima ya afya  ,REHANI ATHUMANI amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa mpango huo ni kumrahisishia mwananchi kupata  huduma ya afya kwa bei nafuu.

MWISHO

No comments:

Post a Comment