Thursday, January 16, 2014

MUNDE AZIDI KUTEKELEZA AHADI YA KUWAINUA WANAWAKE KIUCHUMI TABORA


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tabora Bi.Munde Tambwe akishuhudia diwani wa vitimaalum kata ya Tambukareli Bi.Zinduna akipokea fedha zaidi ya shilingi laki Saba alizozitoa kwa ajili ya kusaidia vikundi vya wanawake wajasiliamali.
Mheshimiwa Munde akikata utepe na kuzindua jiwe la msingi la Wanawake wajasiliamali kata ya Tambukareli manispaa ya Tabora.
Mheshimiwa Munde awali alipokelewa na Chipukizi wa kata ya Tambukareli na kuvishwa skafu ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika kata hiyo.
Mbunge wa jimbo Sikonge Bw.Said Nkumba naye alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliomsindikiza Bi.Munde wakati akifanya ziara ya kufungua baadhi ya matawi ya UWT manispaa ya Tabora.
Meya wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij akieleza baadhi ya ahadi alizozitekeleza Mheshimiwa Munde ambazo pia zimeleta mafanikio makubwa kwa manispaa ya Tabora.

No comments:

Post a Comment