Monday, January 20, 2014

WAAOMBA VYUO VYA SIASA KUREJESHWA

Na Lucas Raphael ,Tabora.

Wanaharakati mkoani Tabora  wamemuomba  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mh  Jakaya Mrisho Kikwete kufanya utaratibu wa kurudisha vyuo vya siasa hapa nchini ili wananchi  hasa wanaotarajia kugombea nafasi mbali mbali za uongozi wa siasa  kufundishwa na kupigwa msasa ili kugombea nafasi hizo wakiwa na uelewa wa kutosha.

Wakiongea na waandishi wa habari jana mjini Tabora baadhi ya wanahabari hao walisema kuwa tatizo la kuwa na viongozi wasiokuwa na maadili limekuwa likichangiwa kwa kiasi kikubwa na wagombea wasiokuwa na uelewa wa kutosha  kujiingiza katika siasa na hatimaye kuwapotosha wanachi badala ya kuwaambia ukweli halisi wa mbambo yanavyokwenda.

“Siku hizi siyo kama zamani,kijana anakurupuka kutoka chuo kikuu kwa kuwa ni msomi na wala hajasoma siasa anaenda anagombea nafasi yeyote ya kisiasa na anachaguliwa ,unategemea huyu ambaye hajui siasa hata kidogo ataiambia nini jamii kama siyo kuipotosha? Na hiki dicho chanzo cha kuwapata viongozi wasiokuwa na maadili”alisema mmoja wa wanaharakati hao.

Katika hatua nyingine wanaharakati hao wameeleza kushangazwa na  kitendo cha baadhi ya wanasiasa kupinga kupongezwa kwa Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli Edward Lowassa kutokana na jitihada mbali mbali anazozifanya kwa nchi yake.

Walisema hata nchi zilizoendelea zina utamaduni wa kuwapongeza watu au viongozi waliofanya vitu vya kuigwa ila kwa nchi yetu mtu anapofanya hivyo inaonekana kama kuna nafasi ya kisiasa anayotaka kuiwania kumbe sivyo.

Bwana ,Elisha Daudi  na Deo Kahumbi walisema kuwa ni vema mtu anapostahili pongezi kupewa na kufafanua kuwa Bw Edward Lowassa alionyesha uwezo mkubwa kwa kipindi kifupi cha uongozi wake akiwa kama Waziri mkuu ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa sekondari za kata ambapo sasa asilimia 80 ya wanafunzi wanaomaliza shule ya msingi wanajiunga na sekondari.

Walisema kuwa wakati nchi ilipokumbwa na ukame Lowassa alisimamia kuhakikisha anachi wake wanapata msaada wa chakula hivyo kwa hayo na mengine mengi anayoendelea kufanya hana budi kupongezwa na wanaobeza kupongezwa huko wanaonyesha kutokukomaa kisiasa.

Aidha Bw,Elisha aliongeza kuwa wote  wanaofanya kazi za maendeleo  wanapaswa kupongezwa na siyo kupigwa vita na kuongeza kuwa kipindi cha uchaguzi hakijafika hivyo sasa ni kufanya shughuli za maendeleo tu na kuacha majungu.

MWISHO…………..


No comments:

Post a Comment