Sunday, January 12, 2014

"KUMBE MHESHIMIWA MUNDE HUWA NI MSWEZI!!!''

 
Mbunge wa vitimaalum Bi.Munde Tambwe akionesha umahiri wake katika kucheza ngoma ya Mizimu ya Waswezi ambapo mbunge huyo naye ni Jamii ya Waswezi ambao ni moja kati ya alama zinazoutambulisha mkoa wa Tabora katika historia ya utamaduni wa asili ya Tabora.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora Bw.Emmanuel Mwakasaka akimpatia zawadi Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Tabora Bi.Munde Tambwe wakati akicheza ngoma ya Maswezi huko katika kata ya Tambukareli manispaa ya Tabora.
Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Tabora Mh.Munde Tambwe akitoa salamu na heshima maalumu kwa kiongozi wa Waswezi ikimaanisha kuwa Mbunge huyo naye ni mmoja kati ya Jamii ya watu hao ambao wanahistoria kubwa ya mkoa wa Tabora. 


No comments:

Post a Comment